ThugMaster
JF-Expert Member
- Aug 24, 2015
- 1,594
- 2,234
Daa asante mkuu hapa lipo la kujifunza.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Unamwogopa mwanamke unayeishi naye ndani, unamwamini mwanamme mwingine aliyemuoa huyo ex akulelee mwanao nawe unakenua kwa amani kabisa.... huwezi kuwa sawa kichwani kuna namna dishi limecheza tu.
mwanamke wa ujana wangu anaweza kuwa si yule mama mtoto wanguMaandishi yanasema muoe Mwanamke wa ujana wako.
Hapo ni kweli kabisa. Mimi mke wangu aliniambia kabisa bila kupindisha kwamba nisijaribu kumletea mtoto asie wa tumbo lake, hatokubali kumlea.Hamna mahali popote pameandikwa mwanamke utakae zaa nae ndio unatakiwa umuoe awe mke waako wa ndoa"hakuna".
Ila pia hakuna mahali pameandikwa kwamba mwanamke utakae mzalisha usimpende wala usimpe huduma zote muhimu "hakuna"
Mwanaume unaweza kuwa ulishawahi kuwa na mtoto kwa mwanamke ambae si mkeo kwa sasa so kutokana na kujitambua kwako ukaona uendelee kutoa huduma zote za muhimu kwa mwanao kwasababu unajua fika ile ni damu yako,na hakuna mwingine wa kufanya hivyo zaidi yako.
Bahati nzuri ni kwamba mama mtoto wako (yule x) Anaolewa na mwanaume mwingine na Maisha yao kiuchumi si mazuri. Hata wewe umeona,unaamua kumwomba mama mtoto wako (yule x) umchukue mtoto ili asiteseke unamleta mwanao. Kuja kulelewa na mkeo nyumbani (makosa makubwa sana haya)
Acha nikwambie kitu,
Mkeo hatakwambia simtaki huyo mtoto (ila moyoni mwake kashakwambia)
Mkeo hatokwambia hapendi hata kumuona huyo mtoto (ila moyoni mwake jua hampendi)
Mwanaume wewe unamleta mwanao ukiamini atapata upendo kama wa kwa mama yake (unajidanganya)
Hata kama mama mtoto wako (yule x) utamuona anapitia maisha magumu kwa asilimia 200 usije thubutu mpokonya mtoto. Uje umlete kwa huyu mkeo ulie nae,Pamoja na shida atakazopitia mama mtoto wako (yule x) hatoruhusu shida zile zimpate
Mwanae na hata kama zikimpata mwanao mama yake atajua jinsi ya kumpa maneno mazuri ya kumbembeleza ajione naye yupo kawaida. Wanaume nataka tu muelewe jambo 1 hao wanawake mliowaoa (anakupenda wewe tu) usije jidanganya atampenda.
Mtu mwingine tofauti na wewe na wanae wa kuwazaa. Jitahidi uwezavyo kama una mtoto nnje na ulikua na mpango mwakani (umchukue uje uishi nae), acha maana unamleta jehanam mtoto wako mwenyewe (usijipe moyo kwa matendo yanayofanywa na mkeo ukiwepo) acha huo ujinga.
Muache mtoto wako huko huko kwa mama ake kama ni matumizi mtunze akiwa huko huko kwa mama ake. Kama unahisi unampenda sana huyo mwanao hutaki ateseke (mrudie mama yake muoe). Sasa jitie kichwa ngumu (mletee mkeo mtoto wa mwanamke mwenzie) utaona what next.
Wanawake ndivyoo hivyo walivyo, waelewe then ishi nao kwa akili mingi mingi.
View attachment 1249705
umri huo ni ule umri unaoweza amua wewe kama baba ukasemaHapa sasa nimeelewa kwanini hata Mungu alimtelekeza mwanaye Yesu alelewe na Baba wa kambo, hakutaka kumchukua angali mdogo akasubiri akue.... kwa muktadha huo huo naomba kujua umri wa mtoto kuwa ‘sasa amekua’ kiasi kwamba ‘hatoteseka’ ni upi..?
Wanawake wengi wanataka kuishi na mume wake na watoto wake wa kuzaa. Tofauti na hapo huwa lawamaYaa, mara nyingi wanaume hawana shida na watoto wa kufikia, wanawachukulia tu kama watoto wao wa kuwazaa. Shida ipo kwa mwanamke...
usikubali wala usimsikilize mkeo90% true,binafsi Nina mtoto nilozaa na mwanamke mwingine mbali na uyu Mke nilie nae ila mama wa uyo mtoto kafariki nikapiga esabu akili za wanawake zilivo nikaona nimchukue akakae na bibi Yale kuliko Mke wangu japo yy anasema nimlete kwangu ila hawatabirik hawa viumbe
Mpende mkeo sanaHapo ni kweli kabisa. Mimi mke wangu aliniambia kabisa bila kupindisha kwamba nisijaribu kumletea mtoto asie wa tumbo lake, hatokubali kumlea.
Kweli kabisa mkuu . Its the unspoken truth100% mwanaume mwingine ana uwezo wa kumpenda mwanao kama vile ni wake
ila hamna mwanamke wa kumpenda mtoto wa mwanamke mwingine (tena aliezalishwa na mume wake)
kama wake aliyemzaa.
Uwezo huo wanao wanaume TU.
Je vip kama ume zaa na ex wako alafu yeye nae hakai na mtoto Bali ame mpeleka kijijin kwao huko Ana kaa na bibi yake afu yeye a napambana na maisha ya mume wake Mpyamtoto halelewi na pesa analelewa na MAMA YAKE
wewe unavyomchukua akija nyumbani kwako una uwezo wa kumlea?
au ndio unataka kila ukirudi tu umuone mwanao mbele yako?
Tofautisha "kulea" na "Kukaa na mtoto"
wewe unatetea kukaa na mtoto na wala huna point katika swala la malezi (kulea) ingekua unajua umuhimu wa
KULEA usingebisha mtoto kutunzwa na mama yake aliemzaaaa.
Je vip kama ume zaa na ex wako alafu yeye nae hakai na mtoto Bali ame mpeleka kijijin kwao huko Ana kaa na bibi yake afu yeye a napambana na maisha ya mume wake Mpya
Je na hapa napo uendeelee kutuma pesa kijijin kwa wazaz wa ex wako wakulele au vip?
Mana Kuna wakati sio tuu kuwa na msimamo yenye kuangalia mzingira ya Aina moja pasi Kujua Hali ya upande mwingine
Je vip wale wanawake wanasema wenyewe njoo mchukue mtoto wako mana wapo wanaume wengine hawakubali kulea mtoto WA mtu kama baba yake yupo mjin na anauwezo anamuona hawez kubali hii ime kaaje Nisaidie majibu
Haimaanishi mtoto akilelewa na mwanaume mwingine kisa yuko na mama ake ndio na wewe ubweteke usifatilieZote ni risk sababu huyo mtoto pia yupo kwa baba wa kambo what if baba wa kambo kamfanya mke anamkula mkewe akiwa hayupo au kama wa kiume anaweza kuwa anamuingilia mlango wa uani yani anamlawiti.
Solution ni kuacha kuzaa zaa hovyo kama paka kuwepo na familia ya baba, mama na watoto haikuwa kwa bahati mbaya.
Kuna mdada nilikua nadate nae alinichana kabisa yani kama una mtoto niambie tuachane mapema sitaki dhambi maana haitakaa nimpende nikamwambia sina.