Wanyonge tuunganishe nguvu kumuokoa Diamond

Wamemfanyaje sisi wengine huyu kijana uwa tunamuona kwenye magazeti tu, tumuokoe vipi?
 
Ndiyo kashapotea

Alianza kulalamika ujerumani akaenda uingereza na sasa tanzania......siku si nyingi atalalamikia mbagala

Bora aise maana wake zetu walishataka kutukimbia usiku kisa dayamond kaja mtaani.
 
Hakuna mtu mwenye uwezo wa kuhonga watu elfu moja wamzomee diamond kuna mahala ameharibu ndio maana imekuwa rahisi kwa kundi kumzomea
 

Dah! Umeongea maneno ya elfu mbili. Nimekuelewa mkuu.
Ova
 
Last edited by a moderator:
Hivi Diamond alilazimishwa kutumbuiza Jana???...

Kama alihisi kuna hujuma kulikuwa na ulazima gani wa yeye kurudi kuimba na Davido??..

Na kama sikosei (I stand to be corrected) ilishatolewa taarifa hapa kwamba Ruge Mutahaba(ambaye ni muandaaji mkuu wa FIESTA) ni mmojawapo wa mameneja wa Diamond, pamoja na Babu Tale na Said Fella...Sasa iweje Ruge ashiriki kumhujumu-mtu anayemsimamia???

Mbona watu hamkuunganisha nguvu kumsaidia Lady Jay Dee alivokuwa akifanyiwa unyama na hao Clouds FM kwa mgongo wa Mwana FA???...

Binafsi nakushangaa sana muanzisha thread unaposema Diamond ni icon wa muziki wa Tanzania wakati kuna akina Omary Naliene, Dulla na wenzake kupitia Tatunane , Remmy Ongalla(pamoja na Ukongomani wake), Dk. Hukwe Zawose na wengine walioliletea sifa kubwa sana taifa hili pasipo msaada wa mtandao wala hao wanaoitwa Mameneja..
 
Jamani ifikie wakati tukubali ukweli, Alikiba yuko vizuri lakini diamond amewazidi ubunifu wasanii wote!!! Hutaki unaacha
 
Kiba aliimba... ye hakuzomewa hata kidogo alikua anashangiliwa mwanzo mwisho.... nadhani hata yeye zile shangwe hakuzitegemea..

Diamond arekebishe hizo dharau wanasema anazo otherwise nae ni msanii mzuri sana


diamond katolewa ki muziki na ali kiba na bob junior baadae akaanza kuwatukana..

abadilike
 
diamond katolewa ki muziki na ali kiba na bob junior baadae akaanza kuwatukana..

abadilike

Angeendelea nao asingefika hapo alipo.....wana roho za kimasikini kama za mashabiki wao waliozomeaa...!

Huyo Kiba ndo wa kwanza kupata exposure, alifanya nini cha maana zaidi ya kunata mitaani? Sasa hivi kafulia ndo anapandishwa kwa huruma ya mashabiki...ila sio ubunifu...ooh ana sauti, sauti hata kasuku anayo...

Tunataka kumuona akijituma na tuone ubunifu katika kazi zake...la sivyo ataendelea kuwa msanii wa fiesta tuu huku wenzake wana make money...

Na bado Diamond atawanyima raha sana na roho zenu za korosho.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…