Menejiment yake iangalie upya jinsi yeye almasi anabyofanya kazi zake. Wakuinua kazi zake ni menejiment yake na wao ndio wanaweza kumuangusha.
Kuna vitu mtu anaongea vinaweza kuathiri utendaji wa kazi zake, hasa hawa masupastaa na wanasiasa. Ndio maana wengi huajiri watu wa kuangalia mienendo yao hasa kwenye mitandao ya kijamii., mahojiano na waandishi wa habari na majibizano na wasanii wenzake ambayo kwa hakika hayana tija kwenye kazi zake. Awe na watu wanaomskrutini na kumkanya yapi aseme na yapi asiseme au kujibizana na mtu. Bahati mbaya Mimi sio shabiki wa mziki, hata ukiniuliza ana nyimbo ngapi mwaka huu sina weledi, lakini mtukama almasi ni kioo cha Tanzania na hatuna budi kuinua kipaji chake na kumpa sapoti. Haijalishi wewe ni shabiki wake ama la. Kuna yule dogo alikuwa akija sana jf
heaven on desert, huu ndo wakati wa kufanya kazi ili kuhakikisha chati ya almasi inabaki juu. Tatizo letu watanzania ni wivu. Tunataka wote tuwe masikini.