Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja

Umemmaliza jamaa na pumba zake.

Anataka tuitishe kura ya maoni, huyo wakutisha nani? Kibaraka waliomueka hasa aitishe kura ya maoni watu waamue hatma ya Muungano? Watwambia yale matokeo ya Warioba yamefanyiwa nini?
 

Wazanzibari wengi hawataki mungano. Ukweli kabisa mapinduzi na mungano una masuali mengi bila majawabu. Na ndio maana midahalo ya mambo haya hazarani yamezibitiwa tangu miaka ya 64... hadi leo. Kuna familia zimepoteza wapendwa wao hadi leo kwa kuhoji haya mambo mawili matukufu. Wazanzibari kuwakejeli na kuwazarau kwenye masuali haya ni kutowatendea haki. Vivile ukumbuke kura ya maoni watayarishaji ni watawala na hao hawanashida na mungano wala mapinduzi, mimi huwa nawaita wafalme wa pili wa Zanzibar. Hao wafalme wapili ndio vizazi vyao vina nafasi kubwa kwenye serikali ya zanzibar na ya mungano na wengi wao waligawiwa vitalu Upanga na sehemu nzuri za Dar na hao ndio guardian wa mapinduzi na mungano.
 


Waamue vipi au wapige vipi iyo kura wakati wanatawaliwa kwa mabavu? hawna hata nafasi yakupumua.
Subirini mda utakapofika wakaanza kujifunga mabomu tu nakujiripua mitaani hapa Dar na penginepo ndo mtafahamu kama hawataki.
 
Faith in religion is different from Faith in politics! Pamoja na yooote, Pope anaweza anaweza kuvunja ndoa ikibidi. yeyye tu! Sembuse Muuungano! All sovereign power belongs to the people of Zanzibar and Tanganyika., they are Omega and Alfa of Muungano!
 
Nakubaliana na wewe all the sovereign powers belongs to the people, but if consulted. Jee kwenye muungano, the people of Tanganyika and Zanzibar were consulted?.

Kwenye articles of union, kuna provision yoyote ya kuuvunja muungano tukishindwana?.
Kwa taarifa yako, muungano wetu ni union for life, Tanganyika na Zanzibar, died long ago, Zanzibar limebaki jina, mkivunja muungano mnarudi kuitwa Zanzibar, sisi jee?, tukamfufue Tanganyika aliyekufa na kuzikwa more than 54 years ago?.
P
 
Hakuna kilichokufa, yalibadilika majina tu, nchi bado zipo ukitaka unazitenganisha kama Senegambia ilivyotenganishwa baada ya yaliyotokea.
Paskali, I can assure you Zanzibaris petitioning for the authenticity of Muungano are going to win the case, as you have put it, there was no referendum to determine the same! Wenye sovereignty hawakuulizwa!

Zanzibaris challenge union with Tanzania in regional court
 
Leo Tarehe 26 April, 2020 ni sikukuu ya Muungano, sikukuu hii ndio sikukuu muhimu kuliko hata uhuru kwasababu hii ni siku JMT ilipozaliwa. Lakini kutokana na janga hili la Corona, siku hii inaadhimishwa kimya kimya.
Naawatakia Muungano mwema huku nikisisitiza
Nautakia huu muungano wetu adhimu udumu milele na hivyo kukitokea yoyote anayetaka kuuchokoa muungano, namshauri chokochoko amchokoe pweza, muungano hutauweza kwasababu tutaulinda kwa gharama yoyote.
Nawatakia muungano mwema.
P
 
Nawatakia maadhimisho mema ya sikukuu ya muungano.
Paskali
 
Ni Wakati sasa wa kupiga kura za wazi, kwà wanaotaka muungano waseme ndio na wasio utaka muungano waseme hapana. Ili tupate mahala pa kuanzia.
 
Sasa serikali ya Tanganyika kupitia jina Tanzania inabebeshwa mikopo inayoenda moja kwa moja kuinufaisha Zanzibar lakini Tanganyika itasota kuyalipa na kuweka rehani rasimali zake ili kulipa madeni hayo.
Mkuu Thailand , kuna baadhi ya vitu, mnalalamika bure tuu kwa ujinga wa kutokujua. Elimu kuhusu muungano wetu inahitajika sana.

Kwenye hili la mikopo ya kimataifa, Zanzibar inaruhusiwa kukopa, ila kwasababu Zanzibar sio nchi, hawezi kukopeshwa Zanzibar kama Zanzibar, bali mikopo hiyo lazima idhaminiwe na serikali yetu kwa government guarantee, kwenye government guarantee, huweki rehani kitu chochote!.

Ila ikitokea Zanzibar ikashindwa kulipa, serikali ya JMT ndio itakuwa liable, ila kwa vile Zanzibar is entitled, 4.5% ya fedha zote za misaada ya kimataifa ya maendeleo, ikitokea Zanzibar ikashindwa kulipa deni lolote, JMT italipa, ila nayo itaikata hiyo pesa toka kwenye mgao wao!.

Huu muungano wetu adhimu, tutaulinda kwa gharama yoyote, hata kama baadhi ya gharama hizo ni kuisaidia Zanzibar kulipia madeni yake ya nje, tutalipa tuu.

P
 
Una
Unahisi ulichoandika ni sahihi
 
Tabu ya kupenda mwanamke asiyekupenda . Lazima ugharimikie penzi. Muungano gharama za Tanganyika eti [emoji102]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…