Tatizo kwanini iwe kituo cha polisi, kuna nini hapo?
Haileti picha kamili atakuwa anatafuta kudukua nini?
Mimi nimewahi kukutana na kitu kama hiki, na tena sio Tanzania bali UK, nifufatilie...
Nchi: United Kingdom
Mji:Sheffield
Tukio: Mlevi nje ya sehemu ya maduka.
Mwaka: 2007
Katika eneo hili la maduka, kulikuwa na kituo cha watu binafsi kilichosajiliwa kufanyia mtihani wa nadharia katika mafunzo ya udereva na pia kufanyia mitihani ya kuomba uraia wa Uk.
Kile kituo kwa asilimia kubwa kilikuwa kinahudumia wakaazi wa mataifa mbalimbali na sio waingereza wenyewe sababu hata eneo liilopo ni kunaishi watu wa kutoka Somalia, Yemen, Ethiopina, Eritrea, Iraq, Kenya na wazungu wa ulaya mashariki.
Kwa kuwa haya mataifa, wengi wao wana wazazi watu wazima au pia kuna wale wakaazi ambao bado lugha ya kiingereza kwao imekuwa ngumu kuilewa na kuwa na uwezo wa kuandiaka na kusoma na pia kuwa na uwezo wa kufanya mitihani hiyo.
Mara ghafla wakaanza kuona mlevi mmoja anazagaa zagaa nje ya maduka yao, ambaye alikuwa na asili ya Caribbean(kwa kirahisi tuseme Wajamaica), basi katika pilika zake za ulevi ilikuwa mara kwa mara anaingia ndani ya maduka pamoja na ile ofisi akijifanya kuomba hela ndogo ndogo kama senti 50 au shillingi moja ambayo ndio kawaida ya walevi wote huwa wanaombaomba hiko kiwango cha pesa.
Katika pilikapilika zake kila akiingia humo unakuta anapiga chabo nani wako kwenye kompyuta kwa kuangalia haraka haraka, kwa sababu utakuta alikuwa anapewa data zote kutoka watu wa mfumo, kuwa leo kuna bibi au babu wa makamo ya uzee wa miaka 60 kwenda mbele atahudhuria, au mtu wa nchi fulani na fulani ndio leo wamepangiwa hio tarehe kuja kutahiniwa, sasa anakusanya data kwa kila anachokioana, atakaakaa pale masaa kadhaa nje ya maduka huku akijifanya mlevi na kopo yake pombe za kilevi za kule huwa Cider au Strong beer ambazo zina kiwango ch ulevi kuanzia 8%, ambayo hio ndio picha kamili inayomtanbulisha mlevi nchini Uingereza.
Ikapita miezi kama miezi mitatu au minne, Jamaa kila siku kama kawaida yake anahudhuria pale kujifanyafanya mlevi, mpaka wakamzoea kuwa mlevi mbwa, kwa hiyo wakawa hawana wasiwasi nae.
Basi ilitokea siku moja, zilifunga gari za polisi wa kutosha, wakawasomba watu mle ndani ya ofisi na kubeba kompyuta zote.
Kumbe kile kituo kilikuwa kinakula dili na hao waombaji, siku ya kutanihiwa alikuwa anakuja mtu au kijana waliyempanga kuwafanyia hao waombaji mitihani ya nadharia ya udereva au mtihani wa maombi ya uraia.
Kuanzia siku ile na yule mlevi akapotea mazima, mpaka leo na ile sehemu imeshakuwa duka la mtu mwingine, lakini mpaka leo yule mlevi hajaonekana tena maeneo yale.