Kaka hiyo Mwanzo 1: umeisoma mpaka wapi, umejaribu kuisoma yote? Au umesoma mstari mmoja tu?
Hiyo Mwanzo 1 ndio utatu mtakatifu unapojizihirisha wazi kabisa, Hiyo Mwanzo 1, inasema hivi " Hapo mwanzo MUNGU, aliziumba Mbingu na nchi, Hapa hakuna Mkristo hata mmoja anayebisha kuwa Mungu ndiye aliyeumba, swali linakuja hapa Aliumbaje hiyo Dunia,
Mwanzo 1:2 unasema ROHO YA MUNGU ikatua juu ya uso wa maji, hapo ni Dhairi Mungu anaanza kuzigawa Nafsi zake katika uumbaji, kwamba Mungu ndiye aliyeumba, lakini ROHO YAKE NDIYO ILIYOTUA JUU YA USO WA MAJI, hapo kuna Mungu na Roho lakini upo katika umoja japo inaonekana utofauti wa nafsi
Mwanzo 1:3 Mungu AKASEMA, iwe Nuru, Hapa Mungu anatoa NENO na kusema iwe Nuru,
Hivyo kwenye huu uumbaji tunaona MUNGU, ROHO YAKE na kisha NENO lake, MUNGU, ROHO YAKE NA NENO LAKE NI MUNGU MMOJA,
Ukija kwenye Yohana 1:1-4, inasema hivi Hapo mwanzo alikuwako NENO (mwanzo 1:3) na huyo NENO alikuwako kwa MUNGU na huyo NENO ALIKUWA MUNGU, mstari wa 14 (yohana 1:4), unasema na huyo NENO alifanyika Mwili, Akaaa kwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa MWANA PEKEE atokaye kwa BABA amejaa Neema na Kweli
CC:
Red Giant ,
mgen ,
Mango833 ,
mwana2015 , @G' taxi,
Hb wa Ilala