Wapalestina Gaza washangilia Iran kuipiga Israel. Chakula chaanza kupatikana masokoni

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Vifijo vimerindima ndani ya maeneo ya Gaza baada ya Iran kuamua kuipiga Israel kulipiza kisasi shambulio la Israel dhidi yake huko Syria.

Baadhi ya waliohojiwa jimboni humo wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakipigwa huku majirani zao wakikaa kimya.Kama sasa wataanza kuingilia kati kuipiga Israel basi na suluhisho la madhila yao litapatikana mapema.

Iran's attack on Israel stirs admiration among Gaza Palestinians

Wakati huo huo kwa mara ya mwanzo katika kipindi cha miezi sita watu wa jiji la Gaza lillilobomlewa wameona nafuu katika upatikanaji wa chakula katika masoko.Bei za bidhaa zote kama vile nyanya,ngano na viazi zimekuwa zikishuka siku baada ya siku katika siku za karibuni.

West will condemn Iran’s attack, but largely ignore ‘Israeli provocations’

kwa bahati mbaya, mashambulizi yote yamedakwa 99% hayajadondoka, hakuna madhara israel. hii ni habari mbaya mno kwao.
Hakuna uhakika kuwa kweli 99% zimedakwa kweli.
Kitendo cha kujiamini kupiga kwanza si cha kawaida na hakijawahi kutokea.
 
Kupiga unawezapiga tu,inahitaji ujasiri wa aina gani kurusha ngumi kama umekasirika???

iran alifaa kuwa smart kuliko move hii aliyochukua,wanasema wakati mwingine unapewa jina baya ili uuawe.
 
Iran ikiguswa ataeteseka zaidi Israel.

Maana escalation itakayotokea ni ya middle east nzima.

Lebanese Hizbollah, Al Quds Syria,Hamas Gaza, Houthi Yemeni na makundi mengine Iraq na Afghanistan Taliban lazima watahusika.

Unadhani wao watamlenga nani!?

Na waarabu wengi washagoma ardhi na bandari zao kutumika na USA dhidi ya Iran.

Usichukulie hili suala jepesi.

Shambulio la leo alfajiri Yemen,Lebanon na Syria wamerusha maroketi nao.

Jiulize ikija full scale war na hao wakahusika itakuaje?
 
Iran ikiguswa ataeteseka zaidi Israel.
Maana escalation itakayotokea ni ya middle east nzima.
Lebanese Hizbollah,Al Quds Syria,Hamas Gaza,Houthi Yemeni na makundi mengine Iraq na Afghanistan Taliban lazima watahusika.
Unadhani wao watamlenga nani!?
Na waarabu wengi washagoma ardhi na bandari zao kutumika na USA dhidi ya Iran.
Usichukulie hili suala jepesi.
Shambulio la leo alfajiri Yemen,Lebanon na Syria wamerusha maroketi nao.
Jiulize ikija full scale war na hao wakahusika itakuaje??
Hayo makundi yote backup ni iran,akibanwa vyema hutasikia nguvu ya kundi lolote,kuhusu waarabu kugoma ardhi zao kutumika usiwaamini sana waarabu sio viumbe wazuri linapokuja swala kama hili,nadhani unakumbuka hata issue ya gaza hali ilikuwaje.
 
Hata kama wanafadhiliwa na Iran ila hayo makundi yalikuwepo kabla ya Iran kuyafadhili.

Isipokua Iran kayachochea nguvu tu,Hizbollah ina namna ya kujiendesha licha ya kufadhiliwa na Iran,Houthi imekamata serikali ya Yemeni licha ya kusapotiwa na Iran.

Na pia ikitokea mfarangano hayatokaa kimya lazima yafuate bwana mkubwa wao(Iran) atachofanya,mfano leo Iran kashambulia na wao wakashambulia.

Kesi ya Gaza waarabu walisimama na Palestina ila hawakuweza kuingilia indeep kwasababu.

Na waarabu washazinduka kuwa hawako safe kushirikiana na USA.

Ndio maana hata Oman aliikatalia USA kutumia bandari yake dhidi ya houthi.
 
Hayo makundi yote backup ni iran,akibanwa vyema hutasikia nguvu ya kundi lolote,kuhusu waarabu kugoma ardhi zao kutumika usiwaamini sana waarabu sio viumbe wazuri linapokuja swala kama hili,nadhani unakumbuka hata issue ya gaza hali ilikuwaje.
Kumbuka Iran sio mwarabu ni..muhindi
 
Israel anasumbuka na Hamas harafu mnadhani itakua rahisi kuipiga Iran ni kwamba vita vitasimama kama Russia vs Ukraine...
 
Vifijo vimerindima ndani ya maeneo ya Gaza baada ya Iran kuamua kuipiga Israel kulipiza kisasi shambulio la Israel dhidi yake huko Syria.
Baadhi ya waliohojiwa jimboni humo wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakipigwa huku majirani zao wakikaa kimya.Kama sasa wataanza kuingilia kati kuipiga Israel basi na suluhisho la madhila yao litapatikana mapema.

Iran's attack on Israel stirs admiration among Gaza Palestinians

Wakati huo huo kwa mara ya mwanzo katika kipindi cha miezi sita watu wa jiji la Gaza lillilobomlewa wameona nafuu katika upatikanaji wa chakula katika masoko.Bei za bidhaa zote kama vile nyanya,ngano na viazi zimekuwa zikishuka siku baada ya siku katika siku za karibuni..

West will condemn Iran’s attack, but largely ignore ‘Israeli provocations’

Duh, kwani wamekufa wangapi?
 
Kupiga unawezapiga tu,inahitaji ujasiri wa aina gani kurusha ngumi kama umekasirika???

iran alifaa kuwa smart kuliko move hii aliyochukua,wanasema wakati mwingine unapewa jina baya ili uuawe.
Hamna lolote.Iran kapiga na wote wamenywea wanajitafakari.
Mwanamme ukionewa lazima urushe ngumi.Ukikaa kimya unakuwa kama mwanamke.
 
Iran ikiguswa ataeteseka zaidi Israel.
Maana escalation itakayotokea ni ya middle east nzima.
Lebanese Hizbollah,Al Quds Syria,Hamas Gaza,Houthi Yemeni na makundi mengine Iraq na Afghanistan Taliban lazima watahusika.
Unadhani wao watamlenga nani!?
Na waarabu wengi washagoma ardhi na bandari zao kutumika na USA dhidi ya Iran.
Usichukulie hili suala jepesi.
Shambulio la leo alfajiri Yemen,Lebanon na Syria wamerusha maroketi nao.
Jiulize ikija full scale war na hao wakahusika itakuaje??
Majibu ya kiburi ya Israel mafanikio ya mwanzo kwa Iran ni kupinduliwa kwa Jordan na Jordan ikianguka Israel inamung'unyuka kama mkate.
Iran akiamua kuziba Homutz kama anavyofanya Houth basi nchi zenye mafuta mengi kama Saudia,uae,Kuwait na gesi ya Qattar atazuia zisitoke.Dunia itasimama.
Homutz ni muhimu kwa uchumi wa mafuta kuliko hata Suez Canal ambayo zaidi ni kwa biashara za kimataifa.
 
Na yule King Abdullah watu hawamtaki muache ajichanganye wajomba wafadhiliwe apinduliwe.
Jordan size yake Hizbollah tu wala asiende mbali.
 
mfalme Abdulla mjinga sana.Bora mkewe achukue madaraka.Kama si hivyo Iran achukue madaraka halafu afungue barabara kuvuka mto Jordan.
 
Majibu ya kiburi ya Israel mafanikio ya mwanzo kwa Iran ni kupinduliwa kwa Jordan na Jordan ikianguka Israel inamung'unyuka kama mkate.
Iran akiamua kuziba Homutz kama anavyofanya Houth basi nchi zenye mafuta mengi kama Saudia,uae,Kuwait na gesi ya Qattar atazuia zisitoke.Dunia itasimama.
Homutz ni muhimu kwa uchumi wa mafuta kuliko hata Suez Canal ambayo zaidi ni kwa biashara za kimataifa.
Jordan, Saudi Arabia na Egypt ndizo zinawapa nguvu mazayuni.
 
Back
Top Bottom