Wapalestina ni wavamizi kwa mujibu wa Quran

Ndio ila inatambua kuwa eneo hilo lilikuwa na wenyeji na wala hakuna sehemu ina onyesha wenyeji waliuliwa WOTE, kwahiyo wapo
Mbona hakuna Sehemu huyo Allah aliwarudishia Ardhi WAPALESTINA?

1. Surah Al-Ma'idah (5:21)
"Enyi watu wangu! Ingieni katika ardhi takatifu ambayo Mwenyezi Mungu amekuandikieni, wala msirudi nyuma, msije mkawa wenye kukhasirika."

2. Surah Al-A'raf (7:137)
"Na tukawarithisha watu walio kuwa wanadharauliwa mashariki ya ardhi na magharibi yake, tuliyoibarikia. Na likatimia neno jema la Mola wako Mlezi kwa Wana wa Israili, kwa sababu ya subira yao. Na tukaharibu kabisa waliyo kuwa wakiyatenda Firauni na watu wake na wakayaega."

3. Surah Al-Isra (17:104)
"Na baada ya haya tukawaambia Wana wa Israili: Kaeni katika nchi; na itakapo kuja ahadi ya Akhera, tutakuleteni nyote pamoja."
 
Fahamu kwamba Israel asili yake haikuwa Nchi na haijawahi kuwa Nchi mpaka mwaka 1948 baada ya vita ya pili ya dunia wazungu wa Britain wakalitangaza hilo Taifa la Israel.

Israeli si taifa. Ni jina la Mtume. Nabii huyo ambaye baba yake aliitwa Yakobo, Wana hao wa Israeli walijulikana kuwa makabila 12 ya Israeli. Watu hawa wanaunda wale tunaowaita "Mayahudi" siku hizi, lakini Kiislamu wanaitwa Wana wa Israili, hivyo ndivyo Allah S.W.T anawaita. Neno Israeli halijawahipo kuhusishwa na serikali ni jambo jipya.

Narudia tena Israel ni Jina maalum la Nabii Yakub (AS) alilopewa na Allah (SWT). Haina uhusiano wowote na Nchi ya Kishetani ambayo imelitumia vibaya na kuliteka nyara jina la Nabii wa Mungu.

Umetumia muda mwingi kwenda kwenye Quran tukufu na kuleta hapa baadhi ya aya ingawa ziko na nyengine nyingi umeziacha, lakini katika aya hizo zote ulizoleta na ulizoziacha hakuna mahali zinatafsiri kwamba Israel ni Nchi (State) never (بَنِي إِسْرَائِيلَ) hili neno bani Israel maana yake ni watu wa ukoo Prophet Yakub na si (Nchi/State)

Hao kina Netanyahu na wenzake waliletwa hapo kwenye ardhi ya Palestina kama Diaspora baada ya hiyo vita ya pili ya dunia na kuanza kukatiwa vipande vya ardhi kila siku wanasogea mbele mpaka sasa zamai hizi imefikia halii hii uionayo. na wameletwa hapo kimkakati ili Nchi za ulaya na marekani waweze kupata mahali pa kudhibiti dola za kiarabu (Mashariki ya kati) kutokana na raslimali walizonazo walizobarikiwa lakini pia kujaribu kudhibiti mataifa ya kiislam yenye nguvu duniani na kupenyeza mila zao za kishenzi ili kuwavuruga waislamu.

Nafkiri baada ya kuapta muda kusoma maelezo haya hutakuja tena hapa na kasumba zako kama ulivyolishwa.
Huwa mnamalizia kujenga hoja kijinga sana mkuu,

Nilidhani utakuja na kanusho la aya hizo kwamba hazikuwahusu hao Waisrail, badala yake wewe unaleta hoja ya nchi?

Na mada ni kuwa, kwa mjibu wa Quran inawataja Waisrail ndio walipoewa maeneo hayo, njoo na aya inayokanusha na siyo maelezo ya siyo nchi sjui ikaenda wapi
 
Nilihama siku nyingi baada ya kuujua ukweli, niliukana uislamu pale MSIKITI wa mji mwema ,Kigamboni siku ya ijumaa baada ya Swala
Hongera wana kwa kuijua kweli na kweli imekuweka huru sasa, ndio maana unaiongea kweli na hakuna anayekushinda.
Njia iendayo uzimani ni nyembamba na wachache wataiona.
Mathayo 7:14
Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.
 
Kuna sehemu yeyote katika hizo Aya ulizoziweka ambazo zimewaambia wawafukuze wafilisti (Wapalestina) ambao walikuwa wanaishi hapo?
Hakuna aliyewakataza Waisrael kuishi hapo ila tatizo lao hawawataki Wapalestina yaani waishi wao tu. Hiyo haiwezekani kamwe. Kama hawawezi kuishi na Wapalestina waliowakuta hapo basi wao Waisrael ndio watakao ondoka. Kamwe Wapalestina hawataondoka hapo, hiyo ni ardhi yao milele na milele
 
Kwa mujibu wa Quram Unaongelea juu ya wana wa Israel. Wakati wa Mussa?

Au wana wa Israel wakati wa Yesu

Au wana wa Israel wakati wa Muhamad.

Kwa sababu yesu kazaliwa nchi inayoitwa Palestine

Mussa kazaliwa Masri.

Na kwamba taifa la tanganyika lilikuwapo kabla ya taifa la Israel. Kwa maana hadi mwaka 1967 taifa la Israel halikuwapo.

Kwanini Ethoopia isiwe ndio asili ya Waisrael au sudan kusini
 
Je una Aya kuwa Wafilist waishi hapo pamoja na waisraeli?
 
hakuna hata sura inayosema sisi watanganyika tulipewa hapa tulipo tuishi!!!!

Huwa mnamalizia kujenga hoja kijinga sana mkuu,

Nilidhani utakuja na kanusho la aya hizo kwamba hazikuwahusu hao Waisrail, badala yake wewe unaleta hoja ya nchi?

Na mada ni kuwa, kwa mjibu wa Quran inawataja Waisrail ndio walipoewa maeneo hayo, njoo na aya inayokanusha na siyo maelezo ya siyo nchi sjui ikaenda wapi
Tunaelewa fika Quran imezungumzia ''wana wa Israel'' lakini haijazunguza mahala popote kwamba "Mimi Mungu nimewakatia au nimewapa eneo la Ardhi wana wa Israel na hii ni nchi yao nayo pia itaiwa jina la Israel" Haya maneno ndani ya Quran hakuna.

Nimekuja na hoja ya Nchi kwasababu wewe heading yako inasema Palestina walivamia kwa mujibu wa Quran Lakini huo ushahidi ulioutoa kwenye Quran yamekosekana hayo maneno ya Israel kumilikishwa au kupewa hiyo nchi /ardhi ambayo wenyewe ni wa Palestina.

Nimekupa asili ya jina Israel nani aliitwa lakini umeweka pamba maskio yako. Usijaribu kuchukua aya za Quran na kubadilisha maana ni vibaya sana na haikubaliki . ni bora kukaa kimya.

Sasa kwa mfano kama Quran ndio iliyotaja kuwapa., Nionyeshe basi wapi Tanzania, ama Kenya, Ugnda, Ruwanda, Burundi, Amerika, Nchi za ulaya na mipaka yao wapi ilitajwa kwenye maandiko na wao wamepewa ni eneo lao? iwe maandiko haya ni kwa hilo taifa bandia tu la Israel???
 
Kwa mujibu wa Quram Unaongelea juu ya wana wa Israel. Wakati wa Mussa?

Au wana wa Israel wakati wa Yesu

Au wana wa Israel wakati wa Muhamad.

Kwa sababu yesu kazaliwa nchi inayoitwa Palestine

Mussa kazaliwa Masri.

Na kwamba taifa la tanganyika lilikuwapo kabla ya taifa la Israel. Kwa maana hadi mwaka 1967 taifa la Israel halikuwapo.

Kwanini Ethoopia isiwe ndio asili ya Waisrael au sudan kusini
Tatizo waislamu hamna elimu Dunia,hamtaki kuchunguza historia ,ndio maana mnakubali kirahisi tu kuwa manabii wale wakiyahudi eti walikuwa waislamu,ili Hali historia inawakataa kabisa ,
Qur'an inawataja Wana wa Israel katika nyakati za Musa, Yesu, na Muhammad, ikiwahusisha na urithi wa Yakobo (Israel), si eneo fulani tu. Yesu alizaliwa Bethlehem ya UYAHUDI , na Musa alizaliwa Misri ,lakini Musa ni myahudi Tena KABILA la LAWI, lakini Wana wa Israel ni kabila la kale lenye historia ndefu kabla ya mataifa ya kisasa.

Kudai kuwa Tanganyika ilikuwapo kabla ya Israel ni kukosa muktadha wa kihistoria. Ingawa Israel ya kisasa ilianzishwa 1948, Ufalme wa Israeli ulikuwepo tangu karne ya 10 KK. Hii inamaanisha kuwa Waisraeli walikuwapo maelfu ya miaka kabla ya Tanganyika.

Ethiopia na Sudan Kusini haziwezi kuwa chimbuko la Waisraeli kwa kuwa hazina uhusiano wa moja kwa moja na taifa hilo la kale. Ingawa Ethiopia ina jamii ya Wafalasha (Wayahudi wa Ethiopia), hakuna ushahidi wa kihistoria unaoonyesha kuwa Israeli ilianzia huko. Hivyo, hoja hii haina msingi wa kihistoria, kidini, wala kisayansi.
 
Tunaelewa fika Quran imezungumzia ''wana wa Israel'' lakini haijazunguza mahala popote kwamba "Mimi Mungu nimewakatia au nimewapa eneo la Ardhi wana wa Israel na hii ni nchi yao nayo pia itaiwa jina la Israel" Haya maneno ndani ya Quran hakuna.

Nimekuja na hoja ya Nchi kwasababu wewe heading yako inasema Palestina walivamia kwa mujibu wa Quran Lakini huo ushahidi ulioutoa kwenye Quran yamekosekana hayo maneno ya Israel kumilikishwa au kupewa hiyo nchi /ardhi ambayo wenyewe ni wa Palestina.

Nimekupa asili ya jina Israel nani aliitwa lakini umeweka pamba maskio yako. Usijaribu kuchukua aya za Quran na kubadilisha maana ni vibaya sana na haikubaliki . ni bora kukaa kimya.

Sasa kwa mfano kama Quran ndio iliyotaja kuwapa., Nionyeshe basi wapi Tanzania, ama Kenya, Ugnda, Ruwanda, Burundi, Amerika, Nchi za ulaya na mipaka yao wapi ilitajwa kwenye maandiko na wao wamepewa ni eneo lao? iwe maandiko haya ni kwa hilo taifa bandia tu la Israel???
Tunawaomba Aya inayoonesha WAPALESTINA walipewa hiyo Ardhi na kunyang'anywa hiyo Ardhi, mnaleta porojo tu,

Kuna aya nyingi zinazoonyesha kuwa Wana wa Israel walipewa ardhi maalum na Mungu. Mfano, katika Qur'an (Al-Ma'idah 5:21), Musa anawaambia Wana wa Israel:

"Enyi watu wangu! Ingieni katika ardhi takatifu ambayo Mwenyezi Mungu amekuandikieni, wala msirudi nyuma, msije mkawa wenye kukhasirika."

Aya hii inaonyesha kuwa ardhi hiyo ambayo kihistoria inajulikana kama nchi ya Kanaani ilitengewa Wana wa Israel. Qur'an yenu inathibitisha kuwa ardhi hiyo iliahidiwa kwao na Mungu.

Pia, hoja kwamba Wapalestina ndio wamiliki pekee wa ardhi hiyo inakosa msingi wa kihistoria. , waislamu jitahidini kusoma historia mtagundua mengi , Kabla ya Waarabu wa Kipalestina kuwepo, kulikuwa na mataifa mbalimbali katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na Wayahudi, Wakanaani, na Wafilisti. Hivyo, dai la kwamba ardhi hiyo ilikuwa ya Wapalestina pekee si sahihi kwa muktadha wa kihistoria na wa kidini.
 
Je una Aya kuwa Wafilist waishi hapo pamoja na waisraeli?
Sijaiona hiyo aya, lakini pia sijaona aya inayosema wawafukuze wafilisti. Nachojua Nabii Ibrahim alihamia hapo akitokea Babiloni ambayo leo ni Iraq akaishi hapo pamoja na hao Wafilisti hakuwafukuza na yeye alikuwa ni mgeni aliyekaribishwa. Nabii Ibrahim akazaa watoto na wajukuu hapo hapo Kanaan, mpaka walipohamia Misri wakati wa Nabii Yusuf.
Walipoondoka Misri walirudi tena kule Kanaan walikokuwa babu zao.

Hakuna nchi ya waisrael peke yao hapo kama hawataki waondoke wao kama walivyoondoka na kuhamia Ulaya kwa karne nyingi huko nyuma. Baada ya kupigwa huko Ulaya eti ndio wawafukuze wapalestina. Never. It will never happen
 
Madai kwamba Ibrahim alikuwa mgeni aliyekaribishwa Kanaan si sahihi kihistoria, kwani Wafilisti walifika baadaye. Pia, Israeli ya kale ilikuwepo kama taifa, hivyo kusema hakukuwa na nchi ya Waisraeli ni kupuuza historia. Uhamiaji wa Wayahudi Ulaya hauondoi uhusiano wao wa kihistoria na Kanaan.
 
Tunawaomba Aya inayoonesha WAPALESTINA walipewa hiyo Ardhi na kunyang'anywa hiyo Ardhi, mnaleta porojo tu,
Weye ndiye uliyekuja na hoja kwamba ili Ardhi iwe yako lazima ije na maandiko kwenye Quran ambapo hilo jambo halipo.
Kuna aya nyingi zinazoonyesha kuwa Wana wa Israel walipewa ardhi maalum na Mungu. Mfano, katika Qur'an (Al-Ma'idah 5:21), Musa anawaambia Wana wa Israel:

"Enyi watu wangu! Ingieni katika ardhi takatifu ambayo Mwenyezi Mungu amekuandikieni, wala msirudi nyuma, msije mkawa wenye kukhasirika."
Tafufa mtu akusaidie kutafsiri aya za Qran vizuri Allah anaposema "Enyi watu wangu" huwa kamkusudia nani
Aya hii inaonyesha kuwa ardhi hiyo ambayo kihistoria inajulikana kama nchi ya Kanaani ilitengewa Wana wa Israel. Qur'an yenu inathibitisha kuwa ardhi hiyo iliahidiwa kwao na Mungu.

Pia, hoja kwamba Wapalestina ndio wamiliki pekee wa ardhi hiyo inakosa msingi wa kihistoria. , waislamu jitahidini kusoma historia mtagundua mengi , Kabla ya Waarabu wa Kipalestina kuwepo, kulikuwa na mataifa mbalimbali katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na Wayahudi, Wakanaani, na Wafilisti. Hivyo, dai la kwamba ardhi hiyo ilikuwa ya Wapalestina pekee si sahihi kwa muktadha wa kihistoria na wa kidini.
 
Sasa kwa mfano kama Quran ndio iliyotaja kuwapa., Nionyeshe basi wapi Tanzania, ama Kenya, Ugnda, Ruwanda, Burundi, Amerika, Nchi za ulaya na mipaka yao wapi ilitajwa kwenye maandiko na wao wamepewa ni eneo lao? iwe maandiko haya ni kwa hilo taifa bandia tu la Israel???
Mkuu, umesahau kwamba, hata mitume wa Mungu alijichagulia yeye,

Kusema hivi ulivyoandika, mawazo yako ni kuyapa uhalali na kuhoji ni kwa nini Mungu aliwapa utume baadhi tu ya watu ili hali watu wote ni wake na ilimpasa awape utume wote

Tunapozungumzia Israil katika hali ya Imani na usipesho wake kwa Mwenyezi Mungu, tunazungumzia upendeleo wake Mungu juu ya hao watu

Na tunapozungumzia Mecca, bado tunazungumzia usipesho wa Mungu kwa eneo hilo

Iweje uanze kutolea mifano ya nchi ambazo sio chimbuko lolote la kile Mungu alikifanya sipesho na kwa mapenzi yake?
 
Madai kwamba Ibrahim alikuwa mgeni aliyekaribishwa Kanaan si sahihi kihistoria, kwani Wafilisti walifika baadaye. Pia, Israeli ya kale ilikuwepo kama taifa, hivyo kusema hakukuwa na nchi ya Waisraeli ni kupuuza historia. Uhamiaji wa Wayahudi Ulaya hauondoi uhusiano wao wa kihistoria na Kanaan.
Haya tufanye umeshinda basi. Tusubiri wawaondoe hao wapalestina kama wataweza. Kamwe hawataweza. Ikifika hiyo siku yaani Wapalestina wote wameondolewa pale niite mbwa kabisa.
IT WILL NEVER HAPPEN I'M SURE 💯
 
Back
Top Bottom