Wapalestina ni wavamizi kwa mujibu wa Quran

Wapalestina ni wavamizi kwa mujibu wa Quran

Wenye ardhi ni wenyeji wao walipelekwa pale , mbona logic ndogo sana
Wapi Quran inasema waisraeli waliondoshwa hapo na wakapewa WAPALESTINA

Je Kuna ushahidi wa Quran kuwa wenye Ardhi walikuwa ni WAPALESTINA

Haya MASWALI mnayakwepa sana
 
Wapi Quran inasema waisraeli waliondoshwa hapo na wakapewa WAPALESTINA

Je Kuna ushahidi wa Quran kuwa wenye Ardhi walikuwa ni WAPALESTINA

Haya MASWALI mnayakwepa sana
Mimi naandika kukuonyesha Israel walivyo ingia hapo wewe unaleta habari za kuondoka, uwe unasoma kuelewa sio kujibu
 
Ibrahim hakuwa myahudi hili ndio jambo la msingi , Yesu hakuanzisha Ukristo nyie ndio mmetengeza ukristo na kuhusisha na Yesu
Hizi ni porojo tu,

Ibrahimu hakuwa myahudi ,ila ndio baba wa wayahudi

Yesu alikuwa myahudi na ndiye mwanzilishi wa Ukristo

Labda uje utuambie hapa Yesu alikuwa KABILA gani na alisali dini gani hapa diniani
 
Mimi naandika kukuonyesha Israel walivyo ingia hapo wewe unaleta habari za kuondoka, uwe unasoma kuelewa sio kujibu
Sasa kama waliingia sinimekupa Aya Allah wako aliwaruhusu ,kumbe unakubali waliruhusiwa kuingia hapo
 
Imani ya Uislamu au dini imeanza au kuja na Muhammad,huu ni ukweli ambao hauna shaka ,kabla ya hapo hapajawahi kuwepo hata chembe ya ushahidi kuwa paliwahi kuwepo dini ya Uislamu

Hili ni swali ambalo niliwahoji MASHEIKH siku naukana uislamu ,walikosa ushahidi

Ubudha upo before hata Ukristo, historia yake ipo ,iweje uislamu historia yake ikosekane kabla ya Muhammad,hata ya kuokoteza haipo
Mohamad kaendeleza tu, lakini watu walikuwa wakifundishwa muda mrefu juu ya imani hii ya Mungu mmoja ambaye ameumba kila kitu kwa uwezo wake
 
Sasa kama waliingia sinimekupa Aya Allah wako aliwaruhusu ,kumbe unakubali waliruhusiwa kuingia hapo
Ndio nimekwambia toka mwanza kuwa waisrael pale kiasili sio KWAO , sasa hapa kuna la kupinga tena
 
Ndio nimekwambia toka mwanza kuwa waisrael pale kiasili sio KWAO , sasa hapa kuna la kupinga tena
Kwahiyo Allah alikosea kuwaweka pale ?

Twende pia kwa ushahidi upi wa Quran kuwa pale kiasili ni kwa WAPALESTINA
 
Mohamad kaendeleza tu, lakini watu walikuwa wakifundishwa muda mrefu juu ya imani hii ya Mungu mmoja ambaye ameumba kila kitu kwa uwezo wake
Kaendeleza wapi bana, Muhammad kaja na dini yake ,ambayo ipo tofauti Tena mbalimbali kabisa na manabii waliopita

Utamdanganyaje mtu Muhammad kaendeleza,
 
Kaendeleza wapi bana, Muhammad kaja na dini yake ,ambayo ipo tofauti Tena mbalimbali kabisa na manabii waliopita

Utamdanganyaje mtu Muhammad kaendeleza,
Vingi walisha fanya wengine , hakuna vipya ambavyo mohamadi amekuja navyo, binadamu ni yule yule
 
Kwahiyo Allah alikosea kuwaweka pale ?

Twende pia kwa ushahidi upi wa Quran kuwa pale kiasili ni kwa WAPALESTINA
Allah kupatia au kukosea sio hoja, hapa hoja ya msingi waisrael lile eneo sio lao kiasili , lazima hili tuliweke wazi
 
Kwa mujibu wa Quran Tukufu WALIOPEWA hiyo Ardhi ni Wana wa Israel,hakuna mahali Quran inawatambua WAPALESTINA,kama Kuna Aya zipo nitaomba nisaidiwe maana elimu ni Bahari

Hebu tuangalie Quran inasemaje kuhusu Ardhi kuwa ni ya Wana wa Israeli .

Uislamu Huwa unakwama kwenye historia tu ambayo mara kadhaa imekuwa ikiwaumbua

1. Surat Al-A'raf (7:137)
وَأَوْرَثْنَا الْقَوْمَ الَّذِينَ كَانُوا يُسْتَضْعَفُونَ مَشَارِقَ الْأَرْضِ وَمَغَارِبَهَا الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا ۖ وَتَمَّتْ كَلِمَةُ رَبِّكَ الْحُسْنَىٰ عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ بِمَا صَبَرُوا ۖ وَدَمَّرْنَا مَا كَانَ يَصْنَعُ فِرْعَوْنُ وَقَوْمُهُ وَمَا كَانُوا يَعْرِشُونَ

"Na tukawarithisha watu waliokuwa wakidharauliwa, mashariki ya ardhi na magharibi yake, ambayo tumebariki ndani yake. Na neno zuri la Mola wako Mlezi likatimia juu ya Wana wa Israel, kwa vile walivyosubiri. Na tukaharibu kabisa waliokuwa wakiyatenda Firauni na watu wake na walizokuwa wakizijenga."

2. Surat Al-Isra (17:104)
وَقُلْنَا مِنْ بَعْدِهِ لِبَنِي إِسْرَائِيلَ اسْكُنُوا الْأَرْضَ فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ جِئْنَا بِكُمْ لَفِيفًا

"Na baada yake tukawaambia Wana wa Israel: Kaeni katika ardhi. Na utakapokuja ahadi ya Akhera tutakuleteni nyote pamoja (kutoka sehemu mbalimbali)."

3. Surat Al-Baqara (2:47)
يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ

"Enyi Wana wa Israel! Kumbukeni neema yangu niliyokuneemesheni, na kwamba niliwafadhilisha juu ya walimwengu."

4. Surat Al-Baqara (2:122)

يَا بَنِي إِسْرَائِيلَ اذْكُرُوا نِعْمَتِيَ الَّتِي أَنْعَمْتُ عَلَيْكُمْ وَأَنِّي فَضَّلْتُكُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ

"Enyi Wana wa Israel! Kumbukeni neema yangu niliyokuneemesheni, na kwamba niliwafadhilisha juu ya walimwengu."

5. Surat Al-Ma'idah (5:24-26)

Aya hizi zinaeleza jinsi Wana wa Israel walivyokataa kuingia katika ardhi hiyo kwa hofu ya watu waliokuwa wakiishi humo, na adhabu yao ya kupotea kwa miaka 40 jangwani:

قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِنَّ فِيهَا قَوْمًا جَبَّارِينَ وَإِنَّا لَن نَّدْخُلَهَا حَتَّىٰ يَخْرُجُوا مِنْهَا فَإِن يَخْرُجُوا مِنْهَا فَإِنَّا دَاخِلُونَ ۝ قَالَ رَجُلَانِ مِنَ الَّذِينَ يَخَافُونَ أَنْعَمَ اللَّهُ عَلَيْهِمَا ادْخُلُوا عَلَيْهِمُ الْبَابَ فَإِذَا دَخَلْتُمُوهُ فَإِنَّكُمْ غَالِبُونَ ۖ وَعَلَى اللَّهِ فَتَوَكَّلُوا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ۝ قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِنَّا لَن نَّدْخُلَهَا أَبَدًا مَّا دَامُوا فِيهَا فَاذْهَبْ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَاتِلَا إِنَّا هَاهُنَا قَاعِدُونَ ۝ قَالَ فَإِنَّهَا مُحَرَّمَةٌ عَلَيْهِمْ أَرْبَعِينَ سَنَةً يَتِيهُونَ فِي الْأَرْضِ فَلَا تَأْسَ عَلَى الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ

("Wakasema: Ewe Musa! Hakika humo mna watu wenye nguvu na sisi hatutaingia humo mpaka wao watoke humo. Wakishatoka, basi tutaingia. Watu wawili miongoni mwao waliomuogopa Mwenyezi Mungu na ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha walisema: Waingilieni kwa kupitia mlango, mtakapoingia humo mtakuwa washindi. Na kwa Mwenyezi Mungu mtegemee ikiwa nyinyi ni waumini. Wakasema: Ewe Musa! Hatutaingia humo kamwe maadamu wao wamo. Basi nenda wewe na Mola wako mpigane, sisi tunakaa hapa. Musa akasema: Hakika ardhi hiyo imeharamishwa kwao kwa muda wa miaka arubaini, watatangatanga katika ardhi. Basi usiwaonee huruma hao watu wapotovu.")

Aya hizi zinaeleza historia ya Wana wa Israel na ardhi waliyopewa ,hivo WAPALESTINA ni wavamizi
Ni wavamizi kwenye ardhi ipi? hiyo mipaka ya ardhi waliyopewa wana Isreal inaanzia wapi na inaishia wapi na katika nchi ipi?

Quran imekuja baada ya Biblia na katika Biblia imewekwa wazi kuwa Gaza, Ashdodi, Ashkeloni na miji mingi ya ukanda wa pwani ya Mediterania hazijawahi kuwa urithi wa wana wa Israel kwa mujibu wa mgawanyo ambao Yoshua alipewa na Mungu.
 
Allah kupatia au kukosea sio hoja, hapa hoja ya msingi waisrael lile eneo sio lao kiasili , lazima hili tuliweke wazi
😂😂Kwahiyo Allah alizingua

Hata mm sikatai walikuta watu hapo ,je Allah alikosea kuwapa hilo eneo
 
Ni wavamizi kwenye ardhi ipi? hiyo mipaka ya ardhi waliyopewa wana Isreal inaanzia wapi na inaishia wapi na katika nchi ipi?

Quran imekuja baada ya Biblia na katika Biblia imewekwa wazi kuwa Gaza, Ashdodi, Ashkeloni na miji mingi ya ukanda wa pwani ya Mediterania hazijawahi kuwa urithi wa wana wa Israel kwa mujibu wa mgawanyo ambao Yoshua alipewa na Mungu.
Una maandiko kwenye Quran kuwa hayo maeneo ni ya WAPALESTINA
 
Vingi walisha fanya wengine , hakuna vipya ambavyo mohamadi amekuja navyo, binadamu ni yule yule
😂😂😂Dini ya Uislamu ni dini mpya yenye taratibu zake tofauti kabisa na waliotangulia
 
Hujajibu nilichokuuliza,hao wenyeji , Quran inawatambua?
Ni wapi Quran yako imesema Gaza ni kwa ajilio ya Waisreali???
Maana mgawanyo wa Nchi takatifu baina ya makabila ya Israel uliweka bayana mipaka na Gaza hawakupewa wana wa Israel. Lakini pia usisahau hivo vitabu vyote vya Biblia na qur-an viliandikwa vikiwa na upendeleo kulingana na nani amekiandika.
 
Eti upendeleo ,

Haya wapi Quran inawatambua WAPALESTINA na eneo lao
 
Eti upendeleo ,

Haya wapi Quran inawatambua WAPALESTINA na eneo lao
Ni wapi Quarn imewatambua Wasaudia na nchi yao?

Usikaze fuvu. Palestina ni nchi kama ilivyo Tanzania. kabla ya uhuni wa marekani palestina ilikuwa hadi na sarafu yake na hati yake ya kusafiria. Kinachoongelewa ni wakazi wa Palestina na ardhi ya Palestina. Quran haijawahi kusema ardhi ya Gaza ni mali ya Waisrael. Biblia ndo iliweka wazi kabisa kwamba Gaza siyo ardhi wa Wana wa Israel.
 
Back
Top Bottom