Kwanza tu ni kuweke sawa ni kuwa wewe ni mnafiki wa wazi kabisa.
Katika swala dogo kama hili umeshindwa kujua nan adui na nani mwenzako usimame nae katika kupambania haki ambayo wewe inakuhusu.
Nadhani unakumbuka ile hadithi ya mtego wa panya ulioua kuku, mbuzi, kondoo na ng'ombe na panya ambaye ndie muhusika wa mtego akapona. Lakini panya huyo huyo aliwaonya na kuwashirikisha hawa wanyama wakubwa wamsaidie na walikataa wakiamini huo mtego wa panya hauwahusu.
Anyways kama hauifahamu hiyo story hebu nenda kaitafute uisome uielewe. Utapata ujumbe.
Wewe raia wenzako wanalalamika kunyanyaswa wewe unatetea bila hata chembe ya huruma. Mbona hauna upendo na watanzania wenzako?!
Unakuwa kama Job ndugai akikaa kwenye kiti kile cha uspika anajibu majibu utadhani yeye anamiliki hii Dunia. Acha dharau.
Kama 1000 kwako ni ndogo kuna wenzako wanaitafuta kwa shida sana na hawapo tayari kunyang'anywa hiyo 1000 kiuonevu kwa kisingizio cha sijui kuchangia kodi ya nini sijui. Ni upumbavu.
Hebu jaribu kuwa muungwana wewe.