Mkogoti
TAPELI Mkubwa
- May 3, 2020
- 2,415
- 3,927
Habarini za Asubuhi Bila shaka mu wazima wote wa Afya
Mada yetu ni kuhusu hii kero ya wapangaji ninapokaa hapa yaani imekuwa shida sana Wanaamua tu kukaa uwani wengine hawana hata kazi Wengi ni wanawake unakuta labda mmoja ndio tu anafua au anafangia uwani, lakini sasa wapo njiani na karibu na njia ya kwenda msalani.
Shida ipo unapiga hesabu ukifika msalani ni kumwanga maji weee ili wasisikie mabomu yanayotoka huko Najikaza lakini wapi, nashindwa nawaskilizia labda watatoka lakini wapi?
Na ukishatoka nje basi wote watakaa kimya unawasalimia wote wataitikia basi huyo watakusindikiza mpaka chooni kwa macho wakati huo wapo kimya, unakaa mule usikii wanaongea tena wanabaki kusikilizia kinachotokea msalani kwa kweli na mimi humu najikakamua kweli kweli ili sound isitoke nje. Nisije jifedhesha nabaki nabaki namwaga maji tu,
Kama wewe ni mpangaji Mwenzangu na umesoma huu uzi na umeshanijua basi naomba hii tabia yenu iishe.