Wapelelezi wa Mikoa Watakiwa Kufuatilia kwa Ukaribu Matukio ya Ukatili wa Kijinsia na Watoto

Wapelelezi wa Mikoa Watakiwa Kufuatilia kwa Ukaribu Matukio ya Ukatili wa Kijinsia na Watoto

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Kamishina wa Polisi Jamii (CP), Fausitine Shilogile amewaelekeza wakuu wa upelelezi katika mikoa (RCO) pamoja na madawati ya jinsia kuhakikisha wanafuatialia kwa ukaribu kesi za ukatili wa kijinsia na unayanyasaji wa watoto ili wanapopeleka jalada kwa Mwanasheria wa Serikali liwe na ushahidi unaojitosheleza.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo yaliyoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Nchini (THRDC) kwa kushirikiana na Shirika la CSEMA kwa kuwahusisha maafisa wa kutoka kwenye baadhi ya vyombo vya dola akiwemo maafisa wa Jeshi la Polisi pamoja na Mawakili kutokea ofisi ya mashtaka Nchini, amesema kesi za ukatili wa kijinsia na unayanyasaji kwa watoto zimekuwa zikiachwa kwa maafisa wanaoshughulika na masuala ya madawati ya jinsia.

"Nawaelekeza Wakuu wa upelelezi wa Mikoa mlioko hapa pamoja na madawati haya (madawati ya jinsia) kuhakikisha mnafuatilia kwa ukaribu kesi hizo (kesi za ukatili wa kijinsia) kuna atendensi kesi hizi tumekuwa tukiwaachia watu wa madawati lakini hizi ni kesi ambazo ni 'sireas' lazima tuzisimamie na tuzitekeleze sisi wenyewe ili tunapo ili tunapochukua 'file' au jalada kulipeleka kwa mwanasheria wa Serikali liwe limekamilika na na liwe limeshiba na ushahidi wote" amesema Kamishina wa Polisi Jamii (CP), Fausitine Shilogile

CP Fausitine Shilogile ameongeza kuwa "Haipendezi wala haifurashi kesi inafika mahakamani inafutwa na mara nyingi mimi uwa nasema kuwa kufaulu kwa kesi ndio kufaulu kwako mpelelezi kesi inapofutwa ina maana kwamba haujafanya kitu ambacho kilitakiwa kifanyike kwahiyo tuhakikishe RCO tunasimamia kwa ukaribu sana kesi hizi na zitoe matokeo chanya"

Aidha, amesema kuwa hali ya ukatili wa kijinsia na unayanyasaji kwa watoto bado sio ya kuridhisha akitoa takwimu za mwaka 2021 na 2020, amesema kupungua kwa kiwango cha matukio hayo ni kutokana na jihudi ambazo zimekuwa zikiendelea kufanyika.

"Takwimu za makosa ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto bado si za kuridhisha katika miaka ya hivi karibuni kwani katika kipindi cha Januari Disemba, 2021 Jumla ya matukio 11,499 yaliripotiwa ukilinganisha na matukio 15,870 yaliyoripotiwa kipindi kama hicho mwaka 2020 hii inaonyesha kuwa juhudi zinafanyika za kupambana na matukio haya hadi kupelekea matukio kupunguza", amesema Kamishina wa Polisi Jamii (CP), Fausitine Shilogile

Pia CP Fausitine Shilogile ametoa wito kwa Taasisi na watu binafsi kuwa vita hiyo ya sio ya Jeshi la Polisi pekee bali amehasa kuwepo kwa ushirikiano kutoa elimu na mafunzo kama kama walivyofanya waandaaji wa mafunzo hao ili wananchi wawe na uelewa wa kutosha waweze kutoa taarifa kwenye vyombo vya sheria na ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande waandaaji wa mafunzo hayo Mratibu wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa amesema kuwa dhumuni la kuandaa mafunzo hayo yanayofanyika kwa siku mbili kuazia leo Augosti 17, 2022 katika ukumbi wa Golden Tulip Hotel Jijini Dar es Salaam, yakiwahusisha maafisa kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga, ni kukumbushana kuhusu misingi ya haki za binadamu na kujadili changamoto zilizopo hususani za ukatili wa kijinsia pamoja na ukatili wa watoto ili kushauriana namna bora ya kuzitatua.
 
Wakuu wa upelelezi wa mikoa pamoja na madawati ya jinsia nchini wametakiwa kuhakikisha kuwa wanasimamia kwa karibu upelelezi wa kesi za ukatili wa kijinsia ili kukamilisha ushahidi wa kesi hizo na hatua ziweze kuchukuliwa.
e93064af-aa9e-43bd-8ae5-53d60617c41e.jpg

Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii CP Faustine Shilogile (kushoto) akizungumza na Mratibu Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC, Onesmo Olengurumo katika mafunzo ya ujengaji uwezo kwa Maafisa wa Polisi, waendesha mashtaka na watendaji dawati la jinsia katika Ukumbi wa Golden Tulip Hotel, Dar es Salaam yakiwahusisha maafisa kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga.

Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii CP Faustine Shilogile ametoa kauli hiyo Agosti 17, 2022, Dar es Salaam wakati akizungumza katika mafunzo ya ujengaji uwezo kwa maafisa wa Polisi, waendesha mashtaka na watendaji dawati la jinsia mafunzo ya kushughulikia kesi za ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto.

Amesema changamoto iliyopo ni kuwa kesi hizo zimekuwa zikiachwa kwa watendaji wa madawati ya jinsia kusababisha kutokamilika kwa ushahidi.

Kamishna Shilogile amesema matukio ya unyanyasaji wa kijinsia yamekuwa yakiongezeka, hivyo mafunzo hayo yatawasaidia kuzipata mbinu mbalimbali za kuweza kukabiliana nazo.

“Jeshi la Polisi pamoja na wadu wengine wa haki jinai Tunaendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa ajili ya kukabiliana na matukio haya lakini pia kuahidi ushirikiano ili kuhakikisha jamii yetu inakuwa kwenye usalama kutokana na matukio hayo,” amesema Kamishna Shilogile.

Kwa upande wake Mratibu Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumo amesema mafunzo hayo yatasaidia ni kujenga umoja katika ya vyombo vya usalam na watetezi wa haki za binadamu kuboresha hali ya haki za binadamu nchini.

Amesema kuwa ili kufanikisha kukabiliana na changamoto hizo ni vyema wadau wote wakashirikiana kwa pamoja wakiwemo wananchi ili kuhakikisha haki zinalindwa.

84eb34ae-f544-417c-a5c4-a78107c74cc8.jpg


photo1660749428.jpeg

Mratibu Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu THRDC, Onesmo Olengurumo

Amesema mafunzo hayo yanalenga kukumbushana kuhusu misingi ya haki za binadamu na kujadili changamoto zilizopo hususani za ukatili wa kijinsia pamoja na ukatili wa watoto ili kushauriana namna bora ya kuzitatua.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa mafunzo hayo Mkurugenzi msaidizi ofisi ya taifa ya mashtaka Renatusi Mkude amesema ipo haja kwa watendaji wa vyombo vya haki jinai kupewa mafunzo lengo ni kubadilishana uzoefu ili kutorudia makosa yanayofanyika.

Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili yameanza Agosti 17, 2022 katika Ukumbi wa Golden Tulip Hotel, Dar es Salaam, yakiwahusisha maafisa kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Tanga.
 
Back
Top Bottom