Marufuku kuwaona
2008-05-15 09:14:57
Na Dunstan Bahai
Jeshi la Polisi nchini, limesema halitawaruhusu ndugu wa watuhumiwa wa `uhaini` waliokamatwa kisiwani Pemba kwenda kuwajulia hali mahala wanakohifadhiwa.
Aidha, jeshi hilo limesema ndugu hao wasiwe na wasiwasi kwani ndugu zao wako salama na wakiumwa wanapatiwa huduma za kimatibabu kama binadamu wengine.
Kauli hiyo ilitolewa na Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Bw. Khamis Mohammed Simba, wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu.
Bw. Simba alikuwa ameombwa aeleze waliko watuhumiwa hao na kama ndugu wanaweza kwenda kuwajulia hali.
Alasiri!!!!!!
Mhh...
wamekuwa watuhumiwa wa uhaini?
Kikwete chonde chonde baba acha hii njia sio nzuri kwa usalama wa nchi yetu
Mi niliuliza kwanini huyu jamaa hongelei swala hili wakati yeye ni bingwa msuluhisha maana kenya alienda, comorro alipeleka majeshi na pia ni kuongozi wa umoja wa africa, kwa cheo hico tuu anapaswa awe msatari wa mbele kushugulikia swala hili,
halafu kama hujagundua naona CCm kila mtu ni msemaji mkuu kuhusu swala la mlipuko wa znz. nafikiri hajui kama hili swala limesha kanza kuwa out of hand
Kumbuka pia kuwa alitoa ahadi ya kushughulikia mambo ya zanzibar!
Mnamzungumzia Zee Comedy - anaendelea na usanii wake mwacheni.
YOU WERE AN ASSASSIN THEN,AND YOU ARE AN ASSASSIN NOWMnamzungumzia Zee Comedy - anaendelea na usanii wake mwacheni.
WANAO TUKWAZA NA KUBOA AMANI NI HAO CCMNani alisema kuwa CCM ndio wanalinda "amani" ya Tanzania?
nyuma ya tukio hili kuna chama cha CUF, hivi ni sawa wengine waumie kwa maslahi ya wachache?
wanachafua hali ya hewa kwa manufaa binafsi? huwageuzA kila siku wenzao ni kafara
Acheni kuongea pumba. kwa akili zenu kweli mnakubali Pemba ijitenge? mmelogwa nini. ijitenge kwasababu gani? kwasababu wamegundua mafuta pale wafaidi peke yao?au kwasababu ya tatizo dogo tu la muafaka huu ambao unaweza kumalizwa kidiplomasia tu natukaendelea kuishi kwa amani zote. nyie msiwe kama watoto wadogo. sasa huu mziki walioanzisha mi nakwambia wataucheza wenyewe. ni kitu mbaya sana kutaka kujitenga.siku hizi dunia nzima watu wanatafuta kujiunga, wao wanatafuta kujitenga. akili gani hiyo?, badae,watu wa kusini wataamua wajitenge makao yao makuu ya nchi yao yawe mbeya. wakaskazini nao itafika kipindi wataamua yawe mwanza. wachaga nao itafikia kipindi watasema yaleyale ya Chifu Maleale, wawe na nchi yao ya kilimanjaro. badae wapwani watasema,sisi tunataka nchi inayoitwa dsm. huu upuuzi ni aibu kwa watu wenye akili kama watz. hata kama kuna matatizo,tushughulikie kuwa pressurise viongozi wamalize tofauti zao, na sio kuomba kujitenga. yasinge patikana mafuta huko pemba mngekuwa na wazo kama hilo?, na je,kama mna roho chafu kama hiyo nyie wapemba wachache,basi siku nyingi mlikuwa na mawazo hayo moyoni na mlikuwa mnatafuta sababu. sasa mmeipata na mnataka kutimiza azma yenu. kwataarifa yenu, naomba muende polepole na tuheshimiane. KAMWULIZENI MUHAMAD BACAR kule anjourn. atawapa ushauri mzuri sana. hata wao walikuwa na matatizo kama hayohayo ya kwenu. solution waliyoichukua,ilikuwa wrong way. na nyinyi fikirini kwanza kabla yakuamua kufanya huu upuuzi. period.
Kidzogalae, mimi siyo Mpemba tena sijawahi hata kufika Pemba wala Unguja, mimi ni Mtanzania. Msimamo wangu ni UMOJA ndiyo maana naunga mkono hata shirikisha la Afrika Mashariki (hata kwenye ile thread yako ya Mradi wa magadi, nimekushangaa unavyo wachukia wakenya).
Sababu nilizo zitoa hapo juu ndiyo zinazonifanya nitofautiane na wewe. Zisome tena sababu ya 1 mpaka 4. I hate oppressors and racists.