Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 60
Kukamata watu usiku wa manane kwa vile tu ni wafuasi wa CUF au kwa vile wanatokea visiwa vya pemba ni ufashisti kama wa Hitler and CCM should know better.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kukamata watu usiku wa manane kwa vile tu ni wafuasi wa CUF au kwa vile wanatokea visiwa vya pemba ni ufashisti kama wa Hitler and CCM should know better.
Wewe nawe Mheshimiwa. Hivi unaposema Wapemba huwa una maana gani? Wapemba katika ujumla wao au Wapemba unaowapenda wewe? Hivi wewe hujapata kuwaona Wapemba walioshika nafasi kubwa tu za uongozi katika Nchi yetu? Waliokuwa Mabalozi? waliopo katika nafasi za |Utaalamu? Waliopo kufundisha mashuleni. Waliopo wanaotibu wananchi wenzao., Hivi wewe unamaanisha Wapemba gani hao? Unaowalilia? Hivi na sisi tumo humo? Maana na sisi pia tunayo nasaba ya Pemba.Mimi naomba kwa Serikali kutafuta suluhu na muafaka.Kuondoa ubaguzi ni mojawapo ya kuwafanya nao waonekane kuwa ni Wazanzibari au Watanzania halisi.
Wapemba wamebaguliwa tangu enzi za Sultani hadi mapinduzi.Wanadharauliwa nchi nzima na kubaguliwa katika nyanja mbalimbali.
Kama Kikwete ana nia nzuri inabidi ku address suala la Pemba kwa diplomasia ya hali ya juu kwa sababau kamata kamata inaharibu sifa ya nchi yetu.Mojawapo ya urithi ambao anaweza kutuachia baada ya uongozi wake katika nchi hii na Afrika nzima ni kuleta amani ya kweli Zanzibar.
Matatizo ya Zanzibar ni matatizo ya Tanzania.
Kukamata watu usiku wa manane kwa vile tu ni wafuasi wa CUF au kwa vile wanatokea visiwa vya pemba ni ufashisti kama wa Hitler and CCM should know better.
Ah Bi sho we. Sasa mtu akifanya vitendo vya uhaini umpigie dandaro au mahumbwa acheze au umsogezee mipasho asikilize? Waache wapate funzo.
Funzo? Hivi hata swala watu wanafanya za nini kama wamejaa mioyo ya chuki namna hii dhidi ya wenzio?
![]()
Kama Pemba wanalia kiasi hicho Tumbatu watakuwa nafanya nini..?
kwi kwi kwi.... kama wameshindwa kumkamata Chenge na Rostam Azizi basi inaonekana hicho kifua mbele kinatokana na kikohozi cha kifua kikuu na sio kupigwa ngumi mgongoni....
Kwa kweli sioni kama hawa Usalama wa Taifa unania nzuri na Serikali ya Kikwete ila inawezekana kabisa ndani ya huu usalama wa Taifa wamo vitimba kwiri ambao bado wanatumiliwa na mafisadi ili kumpaka matope Muungwana na serikali yake ,kama ni mbinu za kumwangusha kitaifa na kimataifa ndio zimeanza ,maana mafisadi wameapa kula sahani moja na Kikwete wakihakikisha kuwa havuki tena na kuendelea na ngwe ya miaka mitano iliyobakia. Na mbinu zipo za aina nyingi za kumchafua huwezi kujua.
Sasa Wapemba wanajitayarisha kuelekea vituo vyote vya polisi ili wakamatwe ili kuonyesha mshikamano na wenzao hao wanasema kubwa lijalo na itakuwa ni kibarua cha kila siku ilivyokuwa hawana kazi za kufanya.
Ah Bi sho we. Sasa mtu akifanya vitendo vya uhaini umpigie dandaro au mahumbwa acheze au umsogezee mipasho asikilize? Waache wapate funzo.
Lakini, mimi ninachojua ni kwamba, wapemba wanaotaka kujitenga wanatapatapa tu. hawataweza. nafikiri JK akiona mambo yanaenda namna hii,bora awe tu dictator. wewe jamaa unaesema selikali iko kama toiletpaper, hauna adabu.mimi sio mwana ccm lakini sipendezewi na manano ya mtu asokuwa na akili kama wewe. ILA, PEMBA WAJIFUNZE KWA MUHAMAD BAKAR. WA ANJOUN. ni sisi wenyewe tulienda kule kukomboa kile kisiwa. sasa wapemba wasijefikiri tutawaacha wao walete ujinga wao. Naomba kikwete awashughulikie kikamilifu,ndani ya sheria, hawa wahaini. chapa fimbo, hata wakijilipua na mabom,waache wajilipue tu, watachoka na watanyamaza wenyewe. period.

That sound exactly like CCM political analyst, fear and fear. Wewe unacho jali ni kutishia watu kwamba wachapwe viboko, sijui wafanywa nini. Kwani kuna ubaya gani wa kuwasikiliza maombi yao, Tanzania si nchi ya demokrasia bwana, tuwasikilize wapemba kwa nini wanataka kuwa nchi huru.
Kama wana qualify kuwa nchi huru, why not kuwaruhusu?
Baada ya Pemba, Kuna Kigoma, Mtwara, Mafia, n.k Wanadai kujitenga na Unguja kwani waliunganishwa lini?