Mimi maoni yangu kukamatwa hao wapemba ni sawa tu maana wao wanajiita ni waaraabu sasa kama ni waarabu sisi wa nini nimeona mama wa kipemba akiileza kuwa wanafanya mgomo wa kupeleka mazao unguja sasa wanamkobmoa nani maana hata wao wakwama kiuchumi kwani hayo mazao wanapeleka bure tatizo la wapemba ni wabaguzi sana
Wacha kunyooshea vidole wengine ,sijasikia wapemba kujiita waarabu labda wameitwa waarabu au unajichanganya na msemo wa waarabu wa Pemba hata Tabora kuna waarabu ,mbeya wapo waarabu tena wengi kuliko Pemba na Unguja yake au huyajui hata Burundi na Ruanda wapo waarabu.
Hapa kuna watu wanataka kunyongwa au kupotea na kupelekwa kusiko julikana ila CCM wameumbuka ,ndipo waswahili tuna msemo usemao Usihadaike na usiku(kiza) ukanya njiani ,kama polisi wanasema hawana taarifa sawa wakae hivyo hivyo wasiwe na taarifa na kama Kikwete hana habari na akae hivyo hivyo asiwe na habari kwani ndivyo viongozi wa CCM wanapoulizwa husema hawajapata taarifa basi wakae hivyo hivyo taarifa wataipata.
Usalama wa taifa huu ni usalama wa Utawala wa Chama kimoja CCM,mabo yote ya kulipuliwa mabomu,kuunguza transformer kuweka kinyesi kwenye visima vya maji huko Pemba yamefanywa na CCM na waliofanya wanajulikana kwa majina polisi na usalama walipewa taarifa ya wahusika na hakuna alieitwa polisi wala kukamatwa usiku.
Mbinde hizi za kukamata watu usiku zimepitwa na wakati ,wako maraisi na wafalme kama akina Shah wa Irani,Mabutu na wengine wengi ambao walikuwa na nguvu kubwa tu na hakuna aliefikiria kuwa wangeliweza kuangushwa na kupinduliwa chali ,leo hii wako wapi na wao walikuwa hizo kamata kamata ndio zao ,je wamefikia wapi ,CCM na utawala wenu wa kidikteta unakaribia mwisho mambo mnayowafanyia WaPemba hakuna kwa sasa ulimwenguni kote zaidi ya hapa Tanzania ,Pemba inahisabika ni moja katika visiwa vidogo sana vinavyoishi binadamu sasa Taifa kubwa kama Tanzania kukibana kisiwa kidogo tu ambacho ni kasehemu kasichozidi hata kilomita 56 na upana usiozidi kilomita 21 ni uharamia wa hali ya chini kabisa ,serikali imeshindwa kukijenga kisiwa hiki ambacho ndicho kilichotowa fedha ya kununua vyombo vyote vya fahari vilivyoko Zanzibar ,si wa umeme wala maji tokea uhuru hadi Muungano,na lililo baya zaidi ni kila ufikapo uchaguzi mkuu hupigwa na kudhalilishwa kama si waTanzania ,hakuna katika Taifa hili la Tanzania sehemu ambayo wanapigwa kama wanyama na vyombo vya dola ,fisadi Mkapa aliwapandisha vyeo polisi waliosimamia zoezi la kuwapiga watu wa Pemba na hili la sasa Kikwete ajifanye kipofu maana watu hawa hawakwenda kwa siri kwenda kupeleka maoni yao ,walifanya hivyo Balozi wa Marekani alipokwenda Pemba na juzi pia hawakufanya siri kwenda kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa.
Serikali kama ingekuwa na njia njema na watu wa Pemba ingewaita kwenye vyombo vya sheria kwa mwito wa dhahiri kabisa kuliko kuwafuatilia usiku wakidhani WaTanzania ni wale wale wa zamani wa kuchapa usingizi na wasijue lipitalo.
Huu ni udikteta ambao mjeshi Kikwete anaanza kuonyesha kucha zake baada ya kushindwa kuwashughulikia wanaoliteketeza taifa na kuliibia matrilion ya shilingi.
Baada ya kushindwa kwao na mafisadi wanarudi kule kule kwa wanyonge wao na kuanza kuwadhalilisha wakiwa wamelala,Usalama gani huu wa Taifa ,kwenda kuwakamata watu wa pemba ambao wameenda kushitaki katika Jumuia za Kimataifa ,kama kweli watu hawa CCM na Usalama wao wanaona nchi itaharibika mbona majambazi walioko kwenye njia kuu ambao ni juzi tu walimuua mtu wa wa Usalama na pia majambazi wanaoiba mchana hata baada ya kutangazwa vita dhidi yao wameanza kuchomoza tena ,huu ni mkakati wa kuwasulubisha watu wa Pemba kama walivyozoea hakuna cha Usalama wala kuhatarisha amani kwani Tanzania hakuna amani isipokuwa kwa mafisadi tu ndio wanaoishi katika amani na utulivu.