Wapendwa naona kama mwisho wangu umekaribia

Status
Not open for further replies.
Usiache kumuomba Mungu kipindi hiki.Wakati mwingine huwa naamini Mungu anaamua kukupitisha tu kwenye tanuru la moto ili uuone ukuu wake na uwe mwanadamu bora.
 
Ushimen
Mshana Jr
Grahams
OKW BOBAN SUNZU na wengine njoeni msaidien hata ushauri mwanaume mwenzenu
Nimechelewa kuona tag yako Mjukuu...

Hata hivyo nitajitahidi kusoma comments zote za wadau ili nione alichoshauriwa nami nitaongezea ikibidi.

Kwakuwa JF ni pool, nina amini anaweza kushikwa Mkono akapata ajira ya udereva ama ajira za viwandani as nimeona amesoma mechanical engineering Kwa ngazi ya diploma.

Wito wangu, kama Kuna mtu mwenye nafasi ya ajira kwenye hayo maeneo mawili tajwa hapo juu vyema tumsaidie mtoa mada(Wanasema mpe nduguyo ajira badala ya kumpa mkate Kila Siku).

Wakati huu ambao atakuwa anashughulikiwa suala la ajira yake, iwapo itawezekana tumsaidieni japo kiasi kidogo cha fedha ili aweze kununua chakula ili apate kuishi na mtoto wake na Mama yake Mzazi ambao wote ni Wategemezi wake kwasasa
 
Naona uwepo wa tatizo ambalo halijafumbuliwa kwa mujibu wa maelezo yako.Mauzauza nyumbani bila shaka ndiyo chanzo cha anguko lako.Maombi yako kama yanatosha basi huenda ulizembea.Lakini kiukweli wahitaji mtaalam alitazame tatizo kwa kina ili lidhibitiwe kwani hata biashara kwa sasa zaweza kutosaidia.Kilichopandikizwa kwako hakijatolewa na hivyo adui anayekutafuna unaishi naye.
 
Nawaambiaga vijana nyie kuleni bata ila hapa duniani kila mmoja anamda atasota tu,ukiona maisha yamekunyookea sana juwa kuna siku utanyooshwa,ishi na watu vinzuri ili siku ukipitia kwenye msota wawe hata wawili wa kukishika mkono
 
Kasema mke wake kakimbia
 
Nimepata wazo Kuna kiwanda kinaitwa Keds kipo picha ya ndege wanalipa kidogo nafuu na inalipwa Kwa wiki
 
Daaah, alikpata ujasiri gani wa kuondoka mkuu?
 
Pole mkuu kwa changamoto za maisha, nina Imani siku si nyingi utajipata tu changamoto tumeumbiwa sisi sote wanadamu.
 
Ku renew driving license ni gharama kiasi gani kinatakiwa?

Pole sana. Lakini kadri mapambano yanavyozidi kuwa makali, ndivyo ushindi unavyokaribia.

Ondoa kabisa mawazo kwamba mwisho wako umekaribia, "awazavyo mtu nafsini mwake, ndivyo alivyo..."

Zichukulie hizi changamoto zote kama ngazi na darasa la kukuvusha hapa ulipo kwenda hatua nyingine.

Ianze Kwa kujiweka nadhifu, ujikae kinyonge hata kama unapitia wakati mgumu kiasi Gani, zingatia kwamba ni hali ya muda tu na itapita.
 
Mkeo ulimrudisha?
 
Pole Sana mkuu kwa magumu unayopitia.
Mungu akufanyie wepesi uinuke tena
 
Ukiwa unafanya biashara za magendo au dilidili kama zako hizo hutoi risiti na blaablaa jitahidi sana uwe umejiwekea EXIT plan maana hizo biashara huwa hazina lifespan ya kueleweka.

Kama mama yako ameshindwa kutibika arudi alipokuwa mwanzo, uza nyumba hela utakayopata tumia kama mtaji na nyingine ya kujikimu. Au kama unaviwanja uzaa upate pa kuanzia.Hakikisha kabla hujauza unabusiness plan ya kueleweka🤝

Jikaze,hao unaita marafiki wamekupa somo la msingi sana katika maisha. Usije kutegemea mtu yoyote hapa duniani.Ndomaana wengine wakifanikiwa pesa zao wanakula wenyewe maana uliteseka mwenyewe ni haki yako.

Wanasema ACHA KAZI UONE ILIVYOKAZI KUPATA KAZI!!!

Huwa siamini sana kwenye hizi biashara( UCHUUZI) zetu za kibongo za kuiganaigana.Ni bora ukazifanya kama part time tu.Ila kufanya kama ndio tegemeo lazima uwe na channel nyingi sana maana muda wowote umaskini unakuita.

1.unacheti cha MECHANICS- kwanini usiende gereji ukatumie ujizi wako japo mwanzo mgumu ila kama shule ipo ni swala ma muda tu.

2.Unaleseni ya kubeba abiria; kwanini usijitumbukize kwenye kazi ya udereva daladala???

#Jitafakari,chukua hatua!
#kataa ndoa,ndoa ni utapeli!!!
 
Shughulika na mambo yako ya kiroho Kila kitu kitakaa sawa.
 
Tatizo lilianza hapo watu walipokuwa wanafagia uwanjani kwako.
 
Pole sana mkuu kwa changamoto unazopitia.

Ila mkuu kuanzia Sasa usisahau kutoa zaka / sadaka kwa Imani yako, kutoka kwenye kila senti unayoipata.......usipuuze hili nakuhakikishia milango yako itafunguka tena.
 
Reactions: Tsh
Sasa mali na utajiri zitakaporudi(Maana ni suala la muda) usisahau waliosimama na wewe wakati huu na walio kukimbia watakapoanza kurudi na visababu kedekede na tumachozi, usiusahau usaliti wao. Pole sana.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…