Wapendwa naona kama mwisho wangu umekaribia

Status
Not open for further replies.
Kitu pekee Kina wafanya watu wang'ang'ane na ajira kwenye serikali na mashirika ya umma ni swala la ulinzi na usalama tu. maana kuhusu hela serikalini hakuna pesa ya kukutajirisha labda uwe mwizi mwizi. wakunielewa wamenielewa
 
Pole sana Ndg yangu kwa changamoto.Nimepitia huko na Bado naendelea kupambana mambo yamekuwa nafuu kuliko jana.USHAURI wangu ...
Mtangulize sana Mwenyezi Mungu,piga magoti ukiwa mwenyewe Lia na usali,akupe faraja na Amani maishani(mtumaini Bwana kwa Moyo wako wote na wala usitegemee akili zako mwenyewe ,katika shida zako umkiri yeye naye atayanyoosha maisha yako.Kama ni Mkatoliki tafuta Novena ya MTAKATIFU RITA ..
ONYO;kipindi hiki Cha majaribu usithubutu hata kidogo USHAURI wa kwenda kwa waganga
 
mkuu mjasiri na mali ww umefika hapo na kuanguka kwa biashara zako kwa kupuuza kitu kimoja muhimu sana ni ULINZI WA KIROHO ww ulikuwa mweupe hukuwa na ulinzi wa kiroho.. yaani kwenye biashara kuna level ukivuka unaamsha vita na husuda na vijicho toka kwa ndugu,marafiki,jamaa,majirani na wafanyabiashara wenzio huko site pia wachawi wa mji ulipo na ukiwa na ulinzi wa kiroho hawatoweza kukuangusha kama uliyoanguka sasa..inasemwa biashara ni vita hivyo ni lazima uchague upande iwe ni upande wa giza au upande wa nuru kamwe huwezi kusimama katikati au vuguvugu ..ushauri wangu ukipata tena mtaji kabla hujarudi kwenye biashara fanyiwa maombi kwanza kuvunja hizo nguvu hasi kwenye kanisa au mchungaji wa kweli wa mungu (achana na wanaojiita manabii sijui mtume) baada ya hapo anza kunyanyua ulinzi wako wa kiroho penda sana kwa kuacha maovu na maasi,fanya mema pia kusali sana na kufanya ibada,toa sadaka kwa yatima,wazee wasiojiweza,wajane,wagonjwa,maskini na kwa watoto wadogo na funga kazi ni jina la yesu na damu ya yesu hii ndio konki..na haya ndio yatakupa ww ulinzi kiroho upande wa nuru na usiyaache hata baada ya kujipata kibiashara bali zidisha ili ulinzi uendelee kuwa juu kwani mahasidi hawatopata tena upenyo kuvuruga njia yako watakuogopa..usiache kutoa sadaka,kufanya maombi sana na ibada na kusaidia yatima na damu ya yesu kwa imani itakutendea maajabu makubwa kiulinzi kiroho na kimafanikio ukiiamini.. na baada ya kunyanyua ulinzi wako kiroho tafuta mtaji rudi kwenye biashara utaona maajabu yake
 
UPO SHULE (Magumu unayopitia ni ada yako)
 
Hao watu wanaofagia uwanja usiku ndio wenye password yako. Wameibinya.

Fanyia kazi hilo, vinginevyo utapata tabu saana
 
Mimi nadhani kuna sehemu ulikosea, Mungu anataka ujifunze kwanza ili ukirudi juu usirudie makosa zingatia kama kuna binadam wenzio uliwakosea...
 
Pole sana.

Kaskazini ipi? Kama ni mchaga omba support kwa wenzio huwa hawaachi wapambanaji wenzao, Omba support haya ya malikauli. Au waombe kazi.

Usisahau kusafishwa kiroho, umechafuka.
 
Pole sana.

Kaskazini ipi? Kama ni mchaga omba support kwa wenzio huwa hawaachi wapambanaji wenzao, Omba support haya ya malikauli. Au waombe kazi.

Usisahau kusafishwa kiroho, umechafuka.
Mtu anasafishwaje kiroho?
 
Kuna jamaa humu nilimuelewa kuhusu the dark side of business
 
Mkuu pole sana kwa yaliyokukuta, ndio ilivyo dunia na walimwengu. Jikubali na endelea kuwa imara usiruhusu hali ya huzuni na kukata tamaa. Anayekujua na kukupenda ni Wewe mwenyewe.

Hata sisi unaoutushirikisha maumivu yako na sisi tuna maumivu makali kuliko wewe na tumeamua kuwa sugu kwa sababu tumejikubali na kuamini kila situation ni ya Jupita tu.

Haiwezi ikawa giza muda wote ipo siku nuru itachomoza tu. Au sio Ms Aaliyyah?
 
Lakini mnapofanikiwa huwa mnatusahau kabisa sisi, mkipata shida mnataka tu shee matatizo. Anyway sisis huwa tupo tu, na utafanikiwa tu usijali, ila this time usitusahau tena.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…