Wapendwa nimeshikwa na ugonjwa wa ajabu, Sura yangu imeharibika

Wapendwa nimeshikwa na ugonjwa wa ajabu, Sura yangu imeharibika

5b7b72e102ae131b207ac5898bc30485.jpg
8df4616d270815314b367ddb3a2e850d.jpg
 
Wapendwa katika BWANA ..
Ninatatizo kubwa sana na baya ambayo naanza kushindwa kutoka hata nje..!

Siku 2/3 hv zilizopita nilishikwa na ugonjwa flani hv upo kama wale mba wa mgongoni au usoni tofauti yake wao wanakuja moja kwa moja uso mzima maana mba huanza kamoja kamoja hadi zinajaa mwili..

Muonekano wangu umebadirika sana from Handsome to Ugly one nashindwa hata kutoka nje niangalie neema za Allah..

Zinawasha hafu sura inavimba kiasi flani..

Nikikumbuka huu ugonjwa utakua ulianza mwezi wa saba maana ulinishika baadhi ya washkaji from Bara wakaniambia ni MATANGO TANGO so nilinunua (ile unayopaka usoni saluni kisha unanawa baaada ya kusuguliwa) nikapewa na videnge kadhaa lkn sikupona...

Siku moja nikiwa mitaa ya FORODHANI ZENJI nikapata dawa flani inaitwa jiko la shamba nikaitumia ikanisaidia nikapoa..
Sasa wikii hii hawa mba/matangotango hata sijui wanaitwaje wameniamulia hakuna jiko la shamba wala la nyumbani ni muwasho na muonekano wa mamba..

Daaah wapendwa nisaidieni sana jina la dawa nitumie na bei zake au kama yawezekana nitengeneze mwenyewe..

Aksanteni sana ma GT wa Jf..

Wenu
Gentries
Mondray 2017
Mimi ni mwanaume usihadaike na Avatar...!​
Nimependa maandishi mekundu tu.
Pole, paka dawa ya mswaki ya Colgate original. Inaweza kukusaidia
 
Muone daktari naamini atakushauri vizuri kuhusu kuzuia kuwashwa tumia majani ya mti wa nyanya fikicha kisha paka sehemu zenye miwaho yanazuia miwasho
 
Nakumbuka niliwahi kupata tatizo kama lako maeneo ya chini ya shingo kushuka mgongoni.
Nilipata tiba pale Aghakhan Dar. Nakumbuka nilichomwa sindano na nikapewa dawa ya kupaka sikumbuki jina. Nilipona kabisa mkuu.
 
Tumia mafuta ya nazi original tengeneza mwenyewe. Mi niliwahi kuugua ugonjwa kama huo na mafuta ya nazi yamenisaidia sana
 
Hii ni Alerg nenda hospital,umekula samaki kakukataa nini!
 
Ndipo tulifikia sasa watoto wa kiume wanataka kuonekana kama wa kike!! Yaani mwanaume unaogopa kutoka nje kisa sura ina upele?? Aisee!! Haf avatar yako ya kike!! Astaghfilullah!! Dunia inaelekea pabaya sasa!!..
 
Back
Top Bottom