Msidanganyike na hivi vishekeli vya sasa! Huu ndio msimu wake, upatipa haraka! Uchafuzi shekeli humwaga kila kona! Kibubu hutobolewa kabisa ili kupunguza kelele
Huu ni wakati wa ulaji.. Ni wakati wa upigaji ... Kama uchafuzi utafanikiwa.. Basi tambua hali ni tete mwakani
Tujiandae! Tufiche kidogo tusile chote.. Tujiandae kukimbiana mwakani.. Waliotukopesha hata kupitia harambee watataka za kwao za awali ndio zirudi kwanza
Kama kuna kamfereji umefanikiwa kukatega katafutie tank la akiba ili kiangazi kikija una pa kuhemea! Una pa kuponea!
Kama kuna kidem kinakuringia sasa hivi kiambie kabisa! Mwakani sio mbali.. Tutaonana tuu😀
Na kama wewe ni jinsia pinzani usimalize zote kwenye vipodozi na show offs! Sponsors watayeyuka kama barafu juani
View attachment 3455463