Wakuu nimefurahi sana kukutana nanyi tena, hakika kwa siku hizi chache nilikua na simanzi sana kukosa kua nanyi humu jukwaani .
Shukrani za kipekee kwa wanaJf wenzangu walionipigia na kunitumia ujumbe kuniarifu kua sasa Jf yetu ipo hewani.Imenipa moyo sana kuona kumbe ninachofanya ni cha thamani sana, hakika sisi ni familia nawaombeni tusitengane.
Team nzima ya Jf nyinyi ni watu muhimu sana kwa jamii yetu, ni mengi mazuri tunayapata kutoka kwenu, hakika mnayo jazaa kubwa kutoka kwa mungu.
Changamoto ni nyenzo ya kujiimarisha na kuongeza ufanisi zaidi, hata siku moja tusizifanye changamoto kua visingizio vya kuharibika mambo, kwani tukifanya hivyo hakuna chengine tutakachopata kwenye maisha haya zaidi ya kutofanikiwa kwenye kila jambo tunalofanya.
Nawapenda sana ndugu zangu zawadi ya penzi langu kwenu nikuwaleteeni kazi zenye ubora wa hali ya juu.
Msiache kunisahihisha na kunishauri,ile penye makosa tusahihishe na penye mapungufu turekebishe
Kaeni mkao wa kula, kazi nzuri zinakujieni. Siku njema wakuu!!