Wapenzi wa push-ups & squats

Push up nzuri unatakiwa upige deep na taratibu , unashuka chini unatulia halafu unapanda unatulia , ukipiga push up namna hii kwa set utaona matokeo mazuri Sana.
Nakuunga mkono, kuna watu wana chezesha kiuno anajifanya kapiga push ups 100
 
Ni kawaida mzee, hiyo hutokea wakati waa kujinyosha viungo, ukipiga push ups sana viungo vinakomaa, ukirelax vinalia kaaa kaaa
 
Kwa kifaa hiki napiga 50 za na za kwaida 20...
 
Push ups zinasaidia sana maana unafanya sehemu yoyote na muda wowote na squart husaidia mzunguko wa damu vizuri hasa sisi wanaume damu kuzunguka kiunoni na nguvu za kiume
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Wewe ua an expert... Umeelezea vizuri
 
Watu hawajui squart na push ups kwa mwanaume ni muhimu kuliko supu ya pweza
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Ila squating ukipiga nyingi unaweza usiende haja kubwa
 
Aisee nimeanza jion hii haya mazoezi nimepiga push-up 60 kwa mafungu ya kumi kumi na squats nimepiga 60 hvyo hvyo kwa mafungu ya kumi kumi hapa najiona baunsa kifuani hope na kitambi kitaishia
Unajiona baunsa unaweza nyanyua nyumba
 
Nimerudi zoezini pia baada kuona nyama choma na bia inataka dominate, kijani mbele ni push ups kama za anko magufuli
 
Hivi push ups zinaongeza nini naona misuli ya nyuma ya mikono imeongezeka kidogoo

Kwa siku asubuhi na jioni huwa napiga 200
Asubuhi 100 na usiku kabisa 100
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…