Ni ngumu kwa wanachuo kuoana au kudumu kwenye ndoa kwa furaha muda mrefu akiwa wataoana. Sababu haswaa ni hizi.
1. Watu wenye kufanana kiumri, elimu na fani ni vigumu kufikiria kuoana au kufurahia maisha ya ndoa kwa muda mrefu. Wanachuo wanaangukia kwenye hilo kundi.
2. Tabia na maisha ya chuoni yako kimpito sana, yanakosa uhalisia wa kudumu (Fake life). Hata mahusiano yanayoanzia chuoni yanabebwa na mazingira ya chuo, wahusika wakimaliza chuo wanakuwa watu tofauti.
3. Chuo kinawaweka watu pamoja kijamii (hivyo watu wanajenga mahusiano kirahisi sana wakiwa chuoni), baada ya kumaliza chuo karibu kila mtu anasepa zake mbali kuanza maisha mapya au kurejea maisha yake ya awali kabla ya chuo (Na hii huvunja mahusiano).
4. Maisha ya chuo yanatoa uhuru mpana kwa mwanafunzi, kuanzia muda, pesa, tabia, mavazi, malazi, shughuli na tabia. Hili huwafanya vijana kutengeneza mahusiano ya rejareja kirahisi mnoo. Baada ya kumaliza chuo, kijana hurejea upya kwenye jamii yake na uhuru huo hupotea ghafla (jamii nyingi zinaupinga huo uhuru wa kijana), na hapo hapo kuua mahusiano ya rejareja ya kijana aliyoyaanzisha akiwa chuoni.