Ndugu sikatai kazi zangu kukopiwa na kusambazwa kwa wengine, nadhani hiyo ndiyo sababu ya mimi kuanzisha blogi, napingana na wewe pale unapokataa kukubali kazi si yako, pale unapobania hilo chimbo kwa wengine, we ukikopy weka link hapo chini kuwa huu mzigo nimeuvumbulia sehemu fulani, ndivyo tunavyo fanya hivyo, kwenye posti nyingi za hiyo blogi nimeonesha ni wapi nimetolea hizo data, sababu lengo ni kujenga maarifa kwa hoja mwingine yeyote anakuwa na nafasi nzuri ya kupinga au kuunga mkono hoja. Blohi yenyewe inayo posti zaidi ya 100 zenye maudhui tofauti tofauti, wewe umevutiwa na posti hii lakini ukiweka link mwenzako utakutana na nyingine inayomvutia, utanisaidia kufikisha ujumbe kwa wengi, na kunipa moyo wa kuendelea kuposti mada mpya.
Ni hayo tu.