Wapi ndugu zangu waweza uza madini ya Ruby?

talentbrain

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2009
Posts
1,187
Reaction score
760
Amani kwenu wadau wa biashara.

Ndugu zangu huko kijijini wamefanikiwa kuchimba madini ya ruby kwa walivyo niambia, yanakadiriwa kufikia robo tatu ya KG. Ila hawajui wapi wayauze na pia hawana vibali vya uchimbaji maana kwa uwezo wao hawawezi kuwa nao. Pia natambua utata wa kisheria uliopo juu ya umiliki wa madini. maana kwa sheria ya madini iliyopitishwa miaka michache iliyopita hata ukiokota madini uko kwenye kosa kisheria.

Naomba msaada wenu, ni wapi ndugu zangu hawa wanaweza kuuza madini yao kisheria na walipe kodi huku wakipata stahili zao bila kupunjwa??

Nimepitia mitandaoni na kupata bei za kimataifa na inaonesha madini haya yanathamani si haba.... Ila ni wapi wanapoweza kuuza na wasikutana na matatizo ya kisheria?? ni kipi wafanye??

Naweza kuwa nimechanganya madesa katika uandishi wa hoja yangu.... Nisameheni!! Ila dhamira yangu ni kuwasaidia ndugu zangu hawa wasije uza at black market au wakayauza kwa bei ya hovyo kama wazee wetu wakati wa ukoloni walipobadilisha kwa shanga!!

nategemea majibu yatayonisaidia.
 
Tuwasiliane kwa taeatibu zaid nitakuelekeza vizuri na watafanikiwa ...ila kwanza ni ruby Gemstones ama ni ya kwenye mwamba karandam kama ile ya mpwapwa...??
 
Sijaiona!! wanaileta week ijayo. Wameichimba sielewi ni kwenye miamba au kwenye ardhi ya kawaida.....
 
Rubby real gem isiyo na sukari wala crack , Gramu 1 ni zaidi ya Mil 300. Kwa hapa Dsm kuna matapeli ya kufa mtu walishamtapeli mpaka Mama Anna Mkapa sio watu kabisa hao ! Soko zuri lipo Arusha au Tanga kuna wa Thailand wanatoa bei nzuri nao
 
Rubby ya ukweli inapatikana kwenye maji chini kabisa baada ya kutoboa mwamba ila kama ni makpishoni kapishoni yanapatikana juu juu tu kwenye miamba ya juu. Rubby ni madini ghali sanaa...linawaka vizuri sanaa ukilikuta ndio lenyewe lina rangi ya Big G ama ile taa ya nyuma ya gari ikiwaka usiku ndio namna Ruby inavyokuwa . Madini safi sanaa kupigia biashara.
 
Kuuza kisheria kwanza kakate leseni ya kufanya biasha ya madini ua ya mchimbaji madini, kisha peleka madini TRA yakakadiriwe dhamani, kisha lipa kodi, sasa unaweza kuuza popote kisheria,

Lakini kama unataka pesa na si sheria, njoo Arusha mabilioni yapo yanasubiria madini ya aina zote.
 
Hayajachimbwa chini ya maji ni milimani kwenye milima inayotokana na bonde la ufa la East Africa..... Sishangai uwepo wake maana geographically inaeleweka kwanini milima hii imetokea na bonde la ufa limetokea.

Nimetazama bei zake kwenye masoko huko nje ni kubwa sana.... Ila ni lazima iwe imetengenezwa katika maumbo.... ila kwa uuzaji wetu tutauza kama yalivyochimbwa....

Ahsante kwa mawazo yako. Unaweza kunisaidia wapi soko lilipo??
 
Kuuza kisheria kwanza kakate leseni ya kufanya biasha ya madini ua ya mchimbaji madini, kisha peleka madini TRA yakakadiriwe dhamani, kisha lipa kodi, sasa unaweza kuuza popote kisheria,

Lakini kama unataka pesa na si sheria, njoo Arusha mabilioni yapo yanasubiria madini ya aina zote.

Kwa uwezo wa ndugu zangu ambao ni mara ya kwanza wameyapata bado saaana kuweza kukata license ya madini. Pia suala la kupeleka TRA na kukadiriwa ni jema sana kama pia TRA watahusika kutafuta masoko huko yaliko.

Kuhusu kuja kuuza Arusha au popote pale nitaongea na wahusika ila najua jinsi biashara hii ilivyo hatari. Nadhani huyo ataeyahitaji atakuja kuyafuata walipo wachimbaji......

Ahsante ndugu kwa mchango wako.
 
Soko la uhakika ni Arusha ule mtaa nimeusahau jina lakini ntakuambia later na wanunuzi wazuri ni Wathailand . Kwa upande wa Dsm yupo mmoja wa Australia naye mzuri. Cha muhimu wacha yaje kwanza ili uangalie quality kuanzia hapo hakuna kitakacho haribikaa
 
Rubby real gem isiyo na sukari wala crack , Gramu 1 ni zaidi ya Mil 300. Kwa hapa Dsm kuna matapeli ya kufa mtu walishamtapeli mpaka Mama Anna Mkapa sio watu kabisa hao ! Soko zuri lipo Arusha au Tanga kuna wa Thailand wanatoa bei nzuri nao
Kaka ni milioni 300 au umekosea kuandika. Mi navojua carat moja ya ruby ni kama dollar 500. Sasa how comes gram moja imefika mil. 300?
 
Sijakosea nakwambia Gramu 1 gem ya uhakika isiyo na sukari wala crack ni bei kubwaaa. Sijakoseaa
 
Rubby real gem isiyo na sukari wala crack , Gramu 1 ni zaidi ya Mil 300. Kwa hapa Dsm kuna matapeli ya kufa mtu walishamtapeli mpaka Mama Anna Mkapa sio watu kabisa hao ! Soko zuri lipo Arusha au Tanga kuna wa Thailand wanatoa bei nzuri nao

Tatizo lako The Fixer huwa unazidisha kamba. Hata kwenye soko LA nje gramme moja haiwezi kuuzwa kwa bei hiyo.
Usimpe mwenzako matumaini hewa. At least soko LA nje gramme moja ina-range to USD.60,000, na hapo inategemea na quality
 
Last edited by a moderator:
Kaka ni milioni 300 au umekosea kuandika. Mi navojua carat moja ya ruby ni kama dollar 500. Sasa how comes gram moja imefika mil. 300?

Jamaa huwa ana kamba. Alishawahi kusema "mercury nyekundu" inauzwa billions of shillings, wakati hata aina hiyo ya mercury ni myth tu haijawahi kuwepo.

Akikupa story za rupia na madini yaliyoachwa na Wajerumani utachoka mwenyewe.
 
Lazima useme hivyo sababu hujawahi kuishika na wala hujui inapatikana katika mazingira gani kwa utaratibu upi yaani kwa ufupi You know nothing...... Tunazungumzia Ruby umeshaingiza na mambo ya rupia. Kuna mwingine ukikwambia mambo ya rupia anakuambia hivyo vitu havipo ni hadithi tu so tunatofautiana ufahamu katika mambo mengi. Jukumu la kuamini ama kutokuamini ni la kwako msomaji hujashikiwa bastola ukubaliane na hoja hii and vice versa
 
Muwe makini pia mtakao enda kununua msije pigwa mkaja kulalamika huku jf

Ushauri kwa ambaye atavutiwa katika hilo dili hakikisha una servilance ya kutosha na hata uwe na tails kibao au ma sniper , hii biashara kwetu sisi haina tofauti na zile biashara za ngada.. Point ni kwamba hutakiwi kuamini hata kama utapewa pesa mpaka vyote vi balance.
 
Soko la uhakika ni Arusha ule mtaa nimeusahau jina lakini ntakuambia later na wanunuzi wazuri ni Wathailand . Kwa upande wa Dsm yupo mmoja wa Australia naye mzuri. Cha muhimu wacha yaje kwanza ili uangalie quality kuanzia hapo hakuna kitakacho haribikaa

Within a week watakuwa wameyaleta hapa kwangu nami niyaone kwa mara ya kwanza... Then nitayapiga picha na kuwaletea hapa nanyi muyaone. Then after nitaanza mkakati wa kuyatafutia soko. Kuna wengine wamesema soko liko Mozambique, Arusha na Dsm!! Nitafanyia kazi details zako nazozipata. Ahsante kwa mchango wako.
 
Kaka ni milioni 300 au umekosea kuandika. Mi navojua carat moja ya ruby ni kama dollar 500. Sasa how comes gram moja imefika mil. 300?

Kwenye bei nami nimekuwa suprised!! Ila hata hao ndugu zangu nao inaonekana wazi wame over say kiwango cha mzigo.... Nasubiri mzigo.
 
Muwe makini pia mtakao enda kununua msije pigwa mkaja kulalamika huku jf

Ushauri kwa ambaye atavutiwa katika hilo dili hakikisha una servilance ya kutosha na hata uwe na tails kibao au ma sniper , hii biashara kwetu sisi haina tofauti na zile biashara za ngada.. Point ni kwamba hutakiwi kuamini hata kama utapewa pesa mpaka vyote vi balance.

Ofcause biashara hii ni hatari kwakuwa upande wowote kati ya mnunuzi na muuzaji inaweza pigwa. Ila kama taratibu za kisheria zitafuatwa naamini kila mtu atacheka. Kama mzigo ni real na pesa zitatolewa kulingana na uhalisia wa bei sioni tatizo.

katika biashara hii hakuna kuamini mtu.
 
Back
Top Bottom