Wapi nikachangamkie fursa ya mazao kipind hiki cha uhaba wa chakula nchini.

Wapi nikachangamkie fursa ya mazao kipind hiki cha uhaba wa chakula nchini.

Kwenye kutafuta hakunaga mtaji mdogo mkuu, unaanza na chochote ulichonacho mkononi. Mfano, shambani kilo moja ya mahindi sasa hivi inauzwa mpaka shilingi mia nne (400), lakini kilometa chache tu mjini yanauzwa mia 6 (mia6), ukishusha ni kuuza tu! Sasa wewe unacheza na soko kwa sababu mtaji wako ni mdogo, unanunua kijijini hata tani moja tu unapeleka mjini fasta mizunguko kadhaa huku ukisoma kushuka kwa bei wakati huo ukikuza mtaji, usiweke stock kama hauna mtaji wa kutosha zungusha fasta iwezekanavyo huku ukibana sana matumizi usipende kukaa sana mjini wewe ukiuza geuka shamba. Mazao yote maharage na mahindi sasa hivi ni dhahabu ndugu. Kuna watu wanapesa nyingi na wana majummba mjini lakini wanaishi shambani tu, hebu piga hesabu mtu anakopesha mfuko mmoja wa mbolea kwa return ya gunia tatu za mahindi wakati wa mavuno, atahama shambani huyo? ACT NOW, AGGRESSIVELY!
Mkuu hayo mazao ni mavuno mapya au ni ya msimu uliopita?

Sent from my HTC One using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mahindi ya sumbawanga,songea na dodoma yapi ya soko sana?
Soko lipi? Sijaahi kuskia mtu anahoji "haya mahindi ni ya wapi?", millers ambao ndiyo wateja wakubwa wa mahindi hawajali yametoka wapi as long as ni mahindi ambayo "hayajagongwa" na yamehifadhiwaw vizuri, wewe ukiwaw na mahindi ya kutosha watu watatoka Kenya kukufuata, mwaka huu watu mpaka wamegombea wakulima.
 
Safi sana mkuu kwa kushea nasi hapa.

Umetoa mwanga mzuri kwa mtu anayeenda huko kama beginner wa biashara hiyo.

Ila naona mtu akienda na mtaji kidogo, faida hatoina.

-Kaveli-
Kwa iyo mtaji at least kiasi gani ndo naanza kuona faida?
 
Pia kama mko wenye mitaji mikubwa vusheni kwa Kenyatta. Huko unga umekua kitu adimu sana.
 
Nimeangalia muktadha wa nchi yetu kwa hali ya sasa,upungufu wa vyakula muhimu,kutokana na tabia nchi,mvua kuchelewa,wakulima kuchelewa kupanda na ukame ulioikumba nchi miez kadhaa nyuma,bei za bidhaa/mazao kupanda,n.k..nataka niitumie hii kama fursa kwenye upande wa biashara ya mazao,kutoa sehem moja kupeleka nyingine.kununua bei ya chini shamban kuuza eneo lingne kwa bei nzur,NAOMBA MSADA wa mawazo.
Karibu mbeya debe lina wastani w kg 18 linauzwa 6500 karibu ,ndanindani kidogo
 
Wenye mitaji changamkieni fursa hizo.

-Kaveli-
 
Mimi pia nipo mwanza nlitaka nfanye biashara hiyo ya mazao hasa ya mahindi na maharage lakini bado sijapata mwongozo,kwa watu wa kanda ya ziwa ,mji gani unauza mahindi bei nafuu kwa ajil ya kuyaleta kuyauza mwanza mwanza???nsaidien wadau,bei kwa kilo,usafiri na bei ya kuuza kwa mjini
 
Ukubwa au udogo wa faida hutegemea mtaji nawe utauza bei gani.
Huko uliko mahindi ni bei gani?
Huku kwetu ni 350 kwa kilo. Kusafirisha Mara nyingi huwa 100/ per kg.
Do a math
Huku niliko ni 700 hadi 800 per kg
Hii ni bei ya Tabora

Wewe upo sehemi gani?
 
Back
Top Bottom