Wakuu ntangulize shukrani kwa wajuvi wa mambo,nikili tu kwamba mimi somo la history nilikuwa mweupe.
Ila nakumbuka kama vile fuvu la binadam-nyani wa kale linapatikana Afrika mashariki. Olduvai George (mtanikosoa)
Sasa fuvu hili ni wazi ni la mwafrika au mtu mweusi,sasa swali langu ni je fuvu la binadamu nyani mzungu linapatikana wapi?
Je wazungu na wao walipitia mabadiliko hayo,kama ndiyo je historical site au museums za hayo mabaki ziko wapi?
Je kama wao watakuwa hawajajiweka kuwa nyani ni sahihi sisi kuendelea kujidharirisha au na sisi tufute kipengere hicho katika mitaara ya shule zetu?π