Wapi nitapata kazi ya malipo ya 5000 kwa siku?

Dah Mungu afanye wepesi ufanikishe bro
 
Kazi gani hiyo hadi ikamvunja mwana shingo usikute mlikua mnabeba injini ya scania.

Ila Big up sana mwanaume ni kujituma
 
Engine Za Scania! Ilikuwa Vitu Vizito Magunia Ila Toka Siku Ile Nikaona Kusoma Ni Rahisi Ikabidi Turudi Class Tu.

Ila Kujituma Kusizidi Uwezo.
Kazi gani hiyo hadi ikamvunja mwana shingo usikute mlikua mnabeba injini ya scania.

Ila Big up sana mwanaume ni kujituma
 
N
Ni kwa bahkresa mzee??
 
Wakuu naomba mnisaidie connection au sehemu ambayo naweza kupata kazi ya malipo ya kiasi cha shilingi elfu tano kwa siku MWANZA MJINI au ILEMELA kama ipo.

NB: Wakuu hata kazi ngumu za ujenzi pia kama zinapatika naomba mnielekeze nikaombe kazi.
Wengi mnakuja kwa gia hiyo mkishapewa connection mnaleta uduanzi.
 
Njoo Iringa kwenye machai. Tunza tiketi YA BASI nauli unarudishiwa ukifika.
1.nyumba bure
2.maji ya uhakika

Vigezo
1. Miaka 18+
2. Uwe na NIDA namba au cheti cha kuzaliwa au kadi ya mpiga kura au namba ya NSSF AU leseni ya udereva

Kazi ni kuchuma kipato ni kutokana na juhudi ya uvunaji lakni kuna kazi zingine za utunzaji wa mashamba ambazo ni sh 7,000/= kwa siku. Kazi ni saa moja kamili hadi saa nane mchana
Hakuna rushwa yoyote na kazi uhakika.

Kampuni inaitwa Lipton teas and Infusion zamani Unilever.

Pm me na karibu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…