Wapi niweke vya kukaa na wapi niweke vya kuchuchumaa

Nataka kuweka vyoo, naomba ushauri wapi niweke vya kukaa na wapi niweke vya kuchuchumaa kwenye vyumba vifuatavyo

1. Public toilet
2. Watoto
3. Master

Naomba na sababu?
Kumbe unajifanya mjuaji tu! Aibu
 
Kuna ndugu yangu yangu ndani ya choo kaeka vyote cha kukaaa na cha kuchuchumaa kwa pamoja.Hivo ukiingia ni chaguo lako.
 
Mkuu kujifunza kwa wengine hakuna mwisho
Kama mwanaume, ni lazima utimize ndoto zako na za familia yako. Inakuwaje utake ndoto zako tukutimizie sisi vizabizabina tusiojua hitaji la moyo❤ la mkeo na wanao? Ama unataka kutujulisha kwamba hujengi nyumba ya ndoto zako?
 
Choo cha kukaa ni private sana, magonjwa mengi yanapatikana kwenye kuchangia vyoo vya kukaa na vinataka usafi wa hali ya juu...
Public ni bora sana vyoo vya kuchutama..
Na vyakukaa ni bora kwa master room mana matumizi yake ni kwa watu wachache na vinaitaji maji ya kutosha..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…