Wapi niweke vya kukaa na wapi niweke vya kuchuchumaa

Wapi niweke vya kukaa na wapi niweke vya kuchuchumaa

Nataka kuweka vyoo, naomba ushauri wapi niweke vya kukaa na wapi niweke vya kuchuchumaa kwenye vyumba vifuatavyo

1. Public toilet
2. Watoto
3. Master

Naomba na sababu?
Kumbe unajifanya mjuaji tu! Aibu
 
Kuna ndugu yangu yangu ndani ya choo kaeka vyote cha kukaaa na cha kuchuchumaa kwa pamoja.Hivo ukiingia ni chaguo lako.
 
Mimi huwa nikijisaidia kwenye Choo Cha kukaa, mzigo hautoki Hadi natamani kupanda juu ya hicho choo[emoji28]
Mim kusema kwel hua napandaga labda niweke mguu nikae muundo wa squat
IMG_20220107_201253.jpg
 
Mkuu kujifunza kwa wengine hakuna mwisho
Kama mwanaume, ni lazima utimize ndoto zako na za familia yako. Inakuwaje utake ndoto zako tukutimizie sisi vizabizabina tusiojua hitaji la moyo❤ la mkeo na wanao? Ama unataka kutujulisha kwamba hujengi nyumba ya ndoto zako?
 
Choo cha kukaa ni private sana, magonjwa mengi yanapatikana kwenye kuchangia vyoo vya kukaa na vinataka usafi wa hali ya juu...
Public ni bora sana vyoo vya kuchutama..
Na vyakukaa ni bora kwa master room mana matumizi yake ni kwa watu wachache na vinaitaji maji ya kutosha..
 
Back
Top Bottom