Wapi niweke vya kukaa na wapi niweke vya kuchuchumaa

Wapi niweke vya kukaa na wapi niweke vya kuchuchumaa

Ishu ya wabongo na Africa kwa ujumla ni uchafu vyooni.Hivyo vyoo vya kukaa US na Ulaya ndio vyoo vyao.Wenzetu usafi wa vyoo wanazingatia sana.Tatizo letu ni uchafu tu.Binafsi napenda choo cha kukaa unakua comfortable.Imagine una harisha zile movement za toilet kuchuchumaa kila saa unateseka but kikiwa cha kukaa unakua comfortable.
 
Na kusihi kama ifuatavyo.
Public toilet hakikisha inakuwa ya kuchuchumaa, halafu vyoo vya vyumbani hakikisha vinakuwa vya kukaa kwasababu vitakusaidia sana utakapokuwa na maradhi yatakayokupa shida kuchuchumaa, pia uwepo choo cha ziada katika chumba kimojawapo utasaidia pindi mzazi mmojawapo akija kwa ugonjwa na akawa na shida ya kuchuchumaa. Zingatia ushauri huu ipo siku utaukumbuka. Public toilet si nzuri kuwa ya kukaa kwakuwa inatumiwa na watu wengi na sidhani kama kila mtu anaweza kuzingatia usafi ipasavyo.
 
Kiafya nashauri
Choo cha kukaa kiwe kwenye master rooms
Chuchumaa kwenye public toilets.
Kwenye public toilet unapata mtu anakojoa pembeni sehemu ya kukalia mtu unapoingia inabd uanze usafi ndio ukate gogo.

Nmewahi ingia shoppers plaza mikocheni nikakuta vyoo vya kukalia watu wamekojolea juu ni vichafu havifai hakuna tissue hakuna sabuni yaani ni uchafu na kuambukizana magonjwa pasipo sababu za msingi.

Vyoo vya kukaa ni vizuri mno ila vinataka usafi wa hali ya juu.

Kuhusu hoja ya kupata mgeni mgonjwa asieweza kuchuchumaa, unapojenga nyumba jenga room mbili self contained, moja yako na moja ya watoto wako wa kike ambayo on emergency case itatumika kuhudumia mgeni mgonjwa. Au kama uko vizuri weka rooms zote self contained[emoji2]
Well said
 
Vinakera Sana[emoji4]

Afu Kuna kitu madau mmoja kauliza
"Choo Cha kukaa, Unajisafishaje na maj?"

Naona watu wanademka TU humu, hawatak kulijibu Hilo swali[emoji4]
Unatumia shuttuf vile vibomba vya kutawazia. Nyie wa wapi? Ina maana hata hajawahi kusafiri au kulala hotel kubwa kubwa?

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Naamini utakuwa ushaweka ila nitajibu kwa experience yangu tangu mtoto hadi saivi, choo cha kukaa its the best asikudanganye mtu sijui vina uti ama nini, ni usafi tu choo kikiwa kisafi na kikavu muda wote hupati ugonjwa wowote. Hata cha kuchuchumaaa kikiwa kichafu kina magonjwa ndo mana uti nyingi wanawake wanapata vyoo vya bar, makazini etc na ni vya kuchuchumaa, kama public unaweza weka choo cha kukaa na uriner sababu wanaume wengi hawana ustaarabu kwenye kukojoa kutumia vyoo vya kukaa. Choo chochote kikubwa usafi though cha kukaa ni best, a bit expensive, kinapendeza na kila kitu sema kingine mazoea tu kama hujazoea kitu utakiona kibaya tu so i hope ulipata jibu sahihi
 
Naamini utakuwa ushaweka ila nitajibu kwa experience yangu tangu mtoto hadi saivi, choo cha kukaa its the best asikudanganye mtu sijui vina uti ama nini, ni usafi tu choo kikiwa kisafi na kikavu muda wote hupati ugonjwa wowote. Hata cha kuchuchumaaa kikiwa kichafu kina magonjwa ndo mana uti nyingi wanawake wanapata vyoo vya bar, makazini etc na ni vya kuchuchumaa, kama public unaweza weka choo cha kukaa na uriner sababu wanaume wengi hawana ustaarabu kwenye kukojoa kutumia vyoo vya kukaa. Choo chochote kikubwa usafi though cha kukaa ni best, a bit expensive, kinapendeza na kila kitu sema kingine mazoea tu kama hujazoea kitu utakiona kibaya tu so i hope ulipata jibu sahihi
Kikubwa usafi tu. Lakino huu wa uswazi huu bora tu cha kuchuchumaa unaweza ukakaa kwenye mavi ya mtu
 
Wengine sisi wa itonjanda tumezoea vya kuchumaa, hadi vya kukaa tunachuchumaa, hapa nakomenti nimechuchumaa kwenye cha kukaa 😂🤣😂🤣
 
Choo cha kukaa ukiangusha gogo kuna maji yanakuja kukubusu kwenye kinyeo.

Halafu ukimaliza hamna namna ya kujichamba na maji.. kuna mtu kasema pipe.. ila nayo ni tatizo sana, ukiipiga vibaya nguo lazima iloe maji.

Kiufupi choo cha kukaa ni changamoto sana
 
Mimi huwa nikijisaidia kwenye Choo Cha kukaa, mzigo hautoki Hadi natamani kupanda juu ya hicho choo[emoji28]
Yaani nilijuaga niko peke yangu aisee...[emoji23][emoji23]
Uongo dhambi,sipendi kutumia choo cha kukaa kabisa. Case ni hiyo hiyo uloisema,sipatagi 'raha' nikikata gogo nimekaa,kwanza mzigo hautoki utakavyo,wakati wa kujisafisha mateso pia. Ila cha kuchuchumaa yaani najisikia amani nashusha kitu hadi nafsi inaridhika.

Kwa bahati mbaya bwana,miaka ya nyuma niliendaga sehemu ya kulala wageni,nikakuta choo ni cha kukaa,nikaomba nibadilishiwe chumba chenye choo cha kuchuchumaa,mhudumu akasema hamna. Aisee nilipanda juu ya choo ndo nikajisaidia vizuri,ile namaliza nataka nishuke kidogo choo kimegeke[emoji23] kama kilitaka kung'oka hivi.

So cha kuchuchumaa kwangu ndo chaguo namba 1. Nadhani pia inachangiwa na makuzi,sisi tumezaliwa maisha ya kunya umechuchumaa tena ukiwa mdogo sana unachimbiwa kashimo kadogo ndo unashusha mzigo hadi utakapokuwa na uwezo wa kuhimili kutumia choo cha watu wazima (kujongea kwenye mabanzi au magogo membaba kama mistimu).
So vyoo vya kukaa tumevijulia ukubwani sana tena tunakutana navyo mahotelini,n.k.

Ila watoto wa sasa hivi akizaliwa akajua kukaa basi anaanza kutengwa kwenye Poti zao zile kama tuviti. Hivyo kizazi kinalelewa kikiwa na misuli iliyozoea kukaa. Sio kwa sisi zamani ukitaka kunya kama ni mchanga,mama anakutenga kwenye miguu yake katikati unashusha mzigo.
 
Mimi huwa napanda kabisa kukaa hamna.

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
Kiukweli huwa nawaza mengi Sana juu ya vyoo hivi ndiyo maana huwa siwezi kuvikalia.

Watu wana ukurutu kwenye makalio, watu wanahara minyoo, watu wana ugonjwa wa pangusa. Naanzaje kukalia vyoo kama hivi?
 
Nataka kuweka vyoo, naomba ushauri wapi niweke vya kukaa na wapi niweke vya kuchuchumaa kwenye vyumba vifuatavyo

1. Public toilet
2. Watoto
3. Master

Naomba na sababu?
Vya kukaa SIKISHAURI UWEKE MAHALI POPOTE NI RAHISI KUAMBUKIZANA MARADHI YA NGOZI.

Usiweke vya kukaa ,Labda chumbani kwako na mkeo TU.
 
Choo cha kukaa ukiangusha gogo kuna maji yanakuja kukubusu kwenye kinyeo.

Halafu ukimaliza hamna namna ya kujichamba na maji.. kuna mtu kasema pipe.. ila nayo ni tatizo sana, ukiipiga vibaya nguo lazima iloe maji.

Kiufupi choo cha kukaa ni changamoto sana
Hahahaa ukitaka kuondokana na hiyo shida. Kabla ya kukaa weka toilet paper kiasi ili i-cushion the fall of the poo na maji yasitawanyike.

Pia kuhusu bidets (spray chrome or bowl) kama unaziona hovyo kama mimi unaweza kununua smart toilet ila hiki choo bei yake imesisima sana. Hiki wewe unakaa tu kina pad control kinafanya kila kitu jinsi wewe unavyoki-command. Hiki nilinunua pale Morocco kama unaelekea Victoria kuna kampuni ABC Emporio yalipo makao makuu ya Vodacom.
 
Back
Top Bottom