Wapiga debe 30 wakamatwa stendi ya Magufuli

Wapiga debe 30 wakamatwa stendi ya Magufuli

Huwezi kuwa na kitu kizuri/standard ukakifanya local
Sijui umenielewa

Ova

Nilijiuliza kama Stand ya nyabugogo Rwanda haina hao wasumbufu isipokua kampuni inakua na watu wake official wa kupokea abiria, lakini pia Roadport stand ya zimbabwe sikuona usumbufu huo iweje Tanzania?

Tena jiji la Dar sasa imekua kila sehemu maturubai na karatasi za bluu kua ni wamachinga yaani tuvibanda kila sehemu! Unajiuliza machinga anauza laki hadi tano au nne kwa siku? Nchi imegeuka kua local hadi tunatia aibu
 
Hilo zoezi liwe endelevu sasa! Siyo baada ya siku mbili, unakuta kimyaaaaa! Kama kule kwenye ile biashara kongwe inayo wavutia Mabaharia wengi wa nchi kavu.
 
Ukitaka kutawala milele jenga jamii ya watu wajinga na masikini
Kupiga vita umasikini ni kuongeza Wigo wa ajira..

Katika vitu vinavyonihuzunisha sana ni kuona jinsi nchi inavyoporomoka toka kwenye uchumi rasmi wa wastani uliotawaliwa na viwanda na makampuni makubwa ya biashara ambayo ndiyo yalikuwa yanaajiri sehemu kubwa ya wakazi wa Dar hadi kuelekea uchumi usio rasmi wa machinga, mama lishe, bodaboda, gereji bubu, magenge, n.k.

Eti tunaita “kujiajiri; ujasiriamali”. Tunasifu vijana wenye digrii kuendesha bajaji na kuuza genge. Najiuliza, haya mamilioni ya machinga ambao ni vijana chini ya miaka 35 watakuwaje na watakuwa wapi wakigonga 45 na kuendelea? Bado watakuwa barabarani wakining’iniza bidhaa wanazouza kwa wateja kwenye magari? Na watoto wao watakuwa wapi?

Ushauri kwa wakulu wa chama tawala: punguzeni “mdadi” kwenye ma-flyover na madege ya cash; wekeni uzito mkubwa sana kwenye sera ya TANZANIA YA VIWANDA ili kuokoa vizazi vijavyo na dhiki ya kutisha. Ni sera yenu ingawa siku hizi imebakia blabla zaidi. Achaneni na hii porojo ya wasomi kujiajiri kwenye sekta isiyo rasmi.

Mshirika wenu mkuu, CHINA, juzi alitangaza rasmi nchi yao kufanikiwa kutokomeza umasikini - 100%. China sasa haiko tena kwenye kundi la nchi zinazoendelea. Kilichowainua fasta ni kujijengea uwezo mkubwa wa viwanda kiasi cha kuvutia uwekezaji mkubwa toka nchi za Magharibi. Vijana wa kiChina wengi waliandaliwa kitaaluma na wameajiriwa huko; hakuna hizi porojo za kujiajiri kwenye umachinga. Wanajua huwezi kuendeleza nchi kwa shughuli zinazoangamiza taaluma muhimu katika fani za sayansi, teknolojia, ufundi na mikakati ya uchumi kwa ujumla.

Kwa Afrika, Ethiopia, Rwanda na Ghana wameshaanza kufuatilia mkakati wa China.
 
Hayo madebe wanayopiga wakayauze vyuma chakavu wapeta ya kujikimu
 
Kuna siku yaja atawaruhusu na airport waanze kupiga debe napo!!
 
Nilijiuliza kama Stand ya nyabugogo Rwanda haina hao wasumbufu isipokua kampuni inakua na watu wake official wa kupokea abiria, lakini pia Roadport stand ya zimbabwe sikuona usumbufu huo iweje Tanzania?...
Hili jambo linakera sana, unaruhusu vipi watu wanaweka vibanda mpaka kwenye stendi za mabasi alafu abiria wanakosa hata sehemu ya kupumzikia na kujikinga na Jua?!

Unaruhusi vipi wamachinga wanajenga vibanda pembezoni mwa barabara juu ya mitaro ya majimachafu na makaravati , kwenye service roads kiasi kwamba hata watembea kwa miguu wanakosa pakupita na kuingia barabara ya magari,

Hivi ikitokea gari likakosea njia kwa hitilafu yake likavamia vibanda hivyo ni watu wangapi watafariki dunia?! Wengine wanakaanga chips , mihogo au wanapika mama ntilie pembezoni mwa barabara hivi ikitokea gari la mafuta ya petroleum tanker limepata ajali na kulipuka kama pale mbagala au morogoro na mbeya, ni watu wangapi watafariki duniani kwa uzembe tu?!

Tatizo tunaweka siasa mbele na kuruhusu watu wavunje sheria kiasi cha kuhatarisha hata maisha ya watu, tukitarajia kupata wapiga kura wengi kwenye uchaguzi, wanaokaa pembezoni mwa barabara au kuzurura vituo vya mabasi sio wafanyabiashara bali ni vendors!
 
Hamna nisichopenda kama kuvutwavutwa,alafu husipo kuwa makini,ukiwaendekeza wapiga debe unaweza ukapakizwa gari bovu kama safari ya masaa 5 unaweza ukajikuta unatumia masaa 12.
 
Katika vitu vinavyonihuzunisha sana ni kuona jinsi nchi inavyoporomoka toka kwenye uchumi rasmi wa wastani uliotawaliwa na viwanda na makampuni makubwa ya biashara ambayo ndiyo yalikuwa yanaajiri sehemu kubwa ya wakazi wa Dar hadi kuelekea uchumi usio rasmi wa machinga, mama lishe, bodaboda, gereji bubu, magenge, n.k..
Na sisi tutafatilia.

Asante sana mkuu.
 
Back
Top Bottom