henry kilenga
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 1,329
- 1,117
Hapa ndipo utaona jinsi hesabu za ushindi zinavyombeba Lissu! Maana hata katika wale milioni 23 wa mwaka 2015, kuna kundi la watu zaidi ya milioni 5 hawakupiga kura, wengi wao wanatoa sababu kuwa wanakatishwa tamaa kutokana kupiga kura alafu wanatangaziwa kiongozi ambaye hawakumchagua! Lakini mwaka huu chini ya amsha amsha ya Lissu na onyo lake kwa wale watakaochezea maamuzi ya wananchi, kuna mwamko mkubwa wa watu kujitokeza kupiga kura kwa wingi! Watu wana hasira sana na maumivu waliyoyapata miaka hii 5 ya serikali korofi! Hivyo kama haki itatendeka, Lissu atashinda asubuhi! Tuzidi kuwahasisha watu kwenda kupiga kura.
Pia tunavikumbusha vyombo vya dola kwamba watendaji wenu ni waajiriwa wa kiserikali hivyo ajira zao na stahiki zao zote zitaendelea kuwepo hata katika serikali yoyote mpya itakayoingia madarakani, Kwa hiyo hawana sababu ya kutumika kusaidia chama flani kushinda eti kwa hofu ya kukosa ajira kama chama kingine kikishinda, Hilo halipo kabisa! Polisi tendeni haki Muinue taifa!
UFIPA USIOGOPE HAKI ITATENDEKA NA TAIFA LITAINULIWA TUME IKO HURU UTASHINDA KWA KISHINDO PIGA KURA RUDI ULIKOTOKA SHEREKEA USHINDI HAPO ULIPO SAWA