ukiwa na pesa, lazima utakuwa na msimamo na pesa zako. binafsi hata enzi za ujinga kabla sijamjua Bwana, kwasababu sinywi pombe, sijawahi kutoa pesa yangu kumnunulia mwanamke au mtu yeyote pombe. wanawake wengine tulikuwa tunakutana wanaomba niwanyweshe kwanza kabla ya kufanay uchafu lakini nawaambia sumu mojawapo kwanguni pomba, pesa yangu haitakiwi kunnua pombe. ninachoongea hapa, ukiwa na pesa na una imani fulani usingependa pesa/jasho lako litumike kuimarisha jambo ambalo haulipendi, cha msingi wewe tafuta tv zingine uangalie, hao hata usiwalaumu kwanza wamejitahidi sana hata kuweka channel za kikristo, wengine wasingeweka kabisa.
waarabu ni wa ajabu sana kwenye imani, huwaambii kitu. sema kuna mmoja nilikuta kule dodoma, shabiby, kwenye hotel zake hata pombe unapata. nikasema uyu kweli mwarabu wa Gairo. nipo najenga lodge zangu fulani, na humo sitaruhusu pombe kuuzwa, na watakaoingia na kuzini humo lazima watakutana na tangazo kwamba uzinzi ni dhambi.