Mchapafito,
Ningefurahi sana kama tungewakumbuka kwa kuipa mitaa majina yao
kama vile Mtaa wa Tandamuti ulivyobadilishwa na kuitwa Mtaa wa
Mshume Kiyat
Huu ni mfano mmoja.
Jengo la CCM ambalo ndipo yalipokuwa makao Makuu ya African
Association na ndipo palipokuja kuasisiwa TANU nyumba hii ilijengwa
kati ya mwaka wa 1929 - 1933 na ilijengwa kwa kujitolea na viongozi
wa wakati ule.
Baadhi ya viongozi hawa walikuwapo hadi TANU ilipoasisiwa lakini leo
ukiingia katika ofisi za CCM hakuna hata kumbukumbu ya picha zao mle
ndani.
Ikiwa Bunge Dodoma kuna Ukumbi wa
Msekwa kwa heshima ya mchango
wake katika Bunge kwa nini leo tusiwa na ukumbi wa mkutano katika ofisi
kwa kumbukumbu ya
Abdulwahid Sykes au
Earle Seaton au
Sheikh
Hassan bin Amir au
Sheikh Suleiman Takadir.
Ikiwa labda wewe hujapatapo kusikia majina hayo katika kupigania uhuru
wa Tanganyika nakushauri usome kitabu cha
Abdulwahid Sykes.
Ukipenda zaidi ingia hapa:
Mohamed Said: KUTOKA JF: ATHARI YA KUJARIBU KUIBADILI HISTORIA YA TANU NA YA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA