Waliopita huko nyuma sio malaika, ni wanadamu na wanamapungufu yao. Kwa chochote kilichotokea dhana ya kujenga nnchi iliyo na amani, utulivu, upendo na ushirikiano iko mikononi mwetu, wote. Itikadi kali za kidini zilizo na dira ya kuharibu utaifa tulionao ni zakuachana nazo. Keria yangu ya kwanza ilikua ni Upadre, ila baada ya masomo seminary na baada ya masomo zaidi nlikuja tambua inshu za imani, siendi tena Kanisani, zaidi ya kumuomba Mungu na kujaribu ketenda mema.
Imani za kidini, na imani nyingi tulizonazo ni vitu vilivyo pandikizwa bila ridhaa zetu. Wewe ni Muislam na mimi Mkristo MR Mohamed Said, na wewe wala mimi na wengine wengi, hatukua Waislam ama Wakristo simply because tulipata kujua ukweli juu ya Dini hizi mbili ndio tukajiunga, La! simple fact ni kua, Wengi wetu ni waislam na wakristo kwakua TULIZALIWA na wazazi Waislam na wazazi Wakikristo na kulelewa kwenye misingi ya dini hizo. Hivyo basi, kulikua na uwezekano wa wewe kua Mkristo na mimi kua Muislam iwapo tungezaliwa na kukulia chini ya wazazi Wakristo/Waislam. Hilo ndilo chimbuko kubwa la imani zetu za dini, wengi wetu, haikua uamuzi wala chaguo letu.