Pasco,
Hayo hayo uliyoandika ungeweza kuyaandika kwa adabu bila kejeli.
Hakika
Mwinjuma Mwinyikambi kapewa mtaa lakini hujui kisa chake.
Mwinjuma Mwinyikambi nyumbani kwake limewekwa bango kuwa
hapa ndipo palipoanzishwa TANU.
Hii si kweli na kama ulivyoandika huu ni uongo.
Lakini zipo sababu za kutaka historia ionyeshe hivyo na waliofanya
hivyo walifanya kwa lengo maalumu na ndiyo sababu wakakoleza
kwa kumpa barabara.
Max Mbwana kapewa mtaa pamoja na
Mshume Kiyate wakati wa
Kitwana Kondo alipokuwa Meya.
Sina hakika kama kibao cha jina kimewekwa.
Uhakika niliokuwanao ni kuwa kibao cha
Mshume Kiyate hadi leo
hakijawekwa zaidi ya miaka 20 sasa.
Wazee wetu hawakupatapo hata siku moja hata kwa mbali kufikiria
kushusha hadhi ya
Mwalimu Nyerere na ndiyo maana hata ilipoandikwa
historia ya TANU mwaka 1981 na wao mchango wao haukuonyeshwa
ikawa
Nyerere ndiye aliyeanzisha TANU wao walibaki kimya hadi wanaingia
kaburini.
Wangetaka wangeuliza mbona sisi tulianza mambo haya na
Abdul Sykes
1950 na
Abdul ndiye aliyemleta
Nyerere kwetu na kutujulisha na tukijua
mipango ya kuunda TANU?
Lakini sisi ni wanungwana tunajua heshima ya fadhila na utu.
Kwetu kusimanga ni mwiko mkubwa sana.
Kiyate Mshume,
Abdul Sykes, John Rupia, Dossa Aziz, Sheikh
Hassan bin Amir kuwataja wachache hawakuchangia juhudi za kudai
uhuru kwa kupiga dufu.
Ikiwa hujui michango ya wazalendo hawa yote nimeyaeleza katika itabu
cha maisha ya
Abdul Sykes.
Kitafute kitabu usome.
Kinapatikana Ibn Hazm Media Centre Bookshop Msikiti wa Manyema
na Mtoro.
Mwisho nataka nikueleze kuwa safari ya
Nyerere UNO ilianza kupangwa
mwakawa 1950 na mtu aliyesaidia sana alikuwa
Earle Seaton kwa ushauri
wa kisheria na
Seaton alikuwa rafiki ya
Abdul Sykes na ndiye aliyemleta
katika siasa za TANU.
Lakini waliosimamia safari lilikuwa Baraza la Wazee wa TANU chini ya uenyekiti
wa
Sheikh Suleiman Takadir na mkusanyaji fedha za safari alikuwa
Idd
Faiz Mafongo.
Huyu ndiye alikuwa mweka hazina wa Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika na
TANU.
Yako mengi lakini kwa sasa tosheka na maelezo haya.
Nahitimisha kwa kukueleza kuwa huo Mtaa wa
Ally Sykes kajipa mwenyewe
na kauita
Ally Sykes Close.
Mtaa huo hakutunukiwa na haupo katika ramani ya jiji.
Pasco,
Nimekuunga katika blog yangu kukuongezea wasomaji na kukuwekea picha za wazee wetu:
Mohamed Said: KUTOKA JF: UHURU UMELETWA NA NYERERE PEKE YAKE WAISLAM WALIPIGA DUFU