Inshallah nitafanya hivo baada ya mfungo wa ramadhan
Kadoda11,
Allahuma Amin.
Katika post kama tatu hivi za mwisho kuna mengi nimeweka
katika historia ya TANU hukuona la kusema ila umekerwa na
kutajwa
Nyerere...
Hujaona chochote hapa chini:
Pasco,
Mimi licha ya kuambiwa nimefanya utafiti na nimesoma nyaraka za
Sykes jalada baada ya jalada karatasi ya kwanza hadi ya mwisho.
Baada ya kumaliza nikaandika kitabu na ndicho kitabu hivi sasa katika
vyuo vingi duniani wanakosomesha African History kinatumika.
Wala simlazimishi mtu kuamini niliyoandika.
Lakini ikutoshe tu kuwa kitabu changu kimefanyiwa ''review,'' na ''journals''
nyingi Ulaya na Marekani na kimo katika Cambridge Journal of African
History na aliyekiingiza humo ni John Iliffe.
Naamini unalijua hili jarida na hadhi yake na unamjua John Iliffe.
John Iliffe ndiye aliyeandika historia ya Tanganyika na katika mlango wa
African Association nyaraka alizotumia kuandika ni nyaraka za Sykes hizi
alipatiwa na Daisy Abdulwahid Sykes ambae alikuwa mwanafunzi wake
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam mwaka wa 1968.
Ikiwa mimi ni muongo basi hata Iliffe ni muongo na Daisy pia ni muongo
yeye na baba yake marehemu Abdul Sykes maana hizo nyaraka ni za
baba yake Mzee Kleist Sykes ambae Daisy ni babu yake.
Lakini ukipenda unaweza kumsoma Daisy katika, ''Modern Tanzanians,''
kitabu alichohariri John Iliffe, Daisy kaandika katika kitabu hiki maisha
ya babu yake, ''Kleist Sykes: The Townsman.''
Yapo mengi lakini tuishie hapa kwa leo.
Pasco,
Unaweza kuingia hapa kusoma zaidi historia ya Tanganyika:
Mohamed Said: KLEIST SYKES (1894 - 1949) KATIKA DICTIONARY OF AFRICAN BIOGRAPHY (DAB) OXFORD UNIVERSITY PRESS, NEW YORK
Nimeshiriki kama mtafiti na mwandishi katika mradi huo wa Dictionary
of African Biography (DAB) ambao ulikuwa ni ushirika kati ya Harvard
na Oxford University Press, New York.
Kadoda11,
Nyerere katajwa mara ngapi?