Wanabodi,
Ninafurahi kuona kampeni za Uchaguzi mkuu wa 2020 zimeanza huku amani ikitamalaki licha ya changamoto za hapa na pale.
Nimefuatilia uzinduzi wa kampeni wa vyama vya CCM, CDM na ACT- Wazalendo na kugundua kuwa Upinzani bado haujajipanga kuchukua dola.
Uzinduzi wao umejawa na ulalamishi na kupiga madongo CCM. Hakuna matumaibi yoyote ya maana kutoka kwao. CDM hawakuweza hata kuwanadi wagombea wa nafasi ya udiwani. Walishindwa hata kumualika mgombea wao wa Zanzibar. Yani mambo ni hovyo.
Upande mwingine mgombea wa CCM alitoa hotuba iliyojaa matumaini, iliyosheheni data na kutoa dira.
Kwa upande wa mgombea wa CCM, hata jinsi alivyosvughulikia ugonjwa wa korona peke yake inatosha kumpigia kampeni
Wapinzani wanasema TBC haiwatendei haki lakini TBC hiyo ikienda kurusha matangazo yao wanafukuzwa. Walisema kuhusu muungano lakini hakuna lolote. Tuwakatae.
#2020 kura kwa John