Uchaguzi 2020 Wapinzani kuweni makini na njama zinazopangwa dhidi yenu

Uchaguzi 2020 Wapinzani kuweni makini na njama zinazopangwa dhidi yenu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Hakikisheni mawakala wenu wanatimiza vigezo vyote na kuapishwa chini ya usimamizi wenu ili kuepuka njama zinazopangwa za kuchomeka mawakala feki watakaosaidia kusaini matokeo feki.

Hakikisheni mnakagua fomu zote za uchaguzi ili kuepuka njama ya kuondoa picha za wagombea wenu, hili jambo linaweza kutokea msipokuwa makini na limetrend somewhere.

Kataeni wagombea wenu kusimamishwa kufanya kampeni kwa siku kadhaa, Mgonja wa Same amesimamishwa kwa siku 14 na Boniphace Jacob wa Ubungo amesimamishwa kwa siku 7 kwa kisingizio cha uzushi cha kukiuka maadili, kuna njama za kuwasimamisha wengine wengi wasifanye kampeni ili kuiokoa CCM.

Nakala: John Mnyika , CHADEMA , bavicha
 
Mwaka huu ushauri na maelekezo ni mengi sana, inaonekana kuna jambo halipo sawa. Huko ubungo sijaona hata picha moja ya savimbi, atachaguliwa vipi na wasiomfahamu?
 
Mwaka huu ata upinzani uungane na upige kampen usiku na mchana awana mgombea wa kumshinda JPM, JPM amewazidi wenzake kwa ubora kwa kiwango kikubwa sana. Upinzani ujipange vizuri kwa 2025.

Mtu mwenye akili timamu hawezi akachagua CCM .
 
Asante kwa angalizo, inabidi upinzani ujipange vya kutosha na waweke intelijensia ya kuaminika ili waweze kupata taarifa zote muhimu dhidi ya njama ovu zinazoandaliwa na tumeccm.

Pia watilie maanani kila ushauri positive wanaopewa katika mitandao na vyanzo mbalimbali vyenye mapenzi mema na uchaguzi huu, kwa kifupi wachukua tahadhari katika kila jambo maana mwisho umekaribia na ni mwisho mwema.
 
Asante kwa angalizo, inabidi upinzani ujipange vya kutosha na waweke intelijensia ya kuaminika ili waweze kupata taarifa zote muhimu dhidi ya njama ovu zinazoandaliwa na tumeccm.

Pia watilie maanani kila ushauri positive wanaopewa katika mitandao na vyanzo mbalimbali vyenye mapenzi mema na uchaguzi huu, kwa kifupi wachukua tahadhari katika kila jambo maana mwisho umekaribia na ni mwisho mwema
Hakika
 
Back
Top Bottom