1. Ujue kwamba kila mtu anayetaka kugombea urais ameona kwamba ana plan zake nzuri zaidi ya kuongoza na kuifikisha Tz mahali pazuri.
2. Magufuli ni mtendaji mzuri, ila ndio namba moja wa kuvunja sheria za nchi, anafanya anavyotaka yeye, haangalii katiba ya nchi inasemaje.
3. Miradi yote mikubwa anayoitekeleza haiaibuni yeye, ilibuniwa na waliomtangulia, yeye anatekeleza tu, na bila hata kupitishwa na bunge kama taratibu za nchi zinavyotaka.
Mradi aliobuni yeye ni daraja la Mfugale na daraja la Salender.
4. Ameminya demokrasia na kutaka kuua vyama vya upinzani kwa gharama yoyote ile.
5. Ameminya uhuru wa wananchi kiasi kwamba hata kama una maoni yoyote tofauti ukiyatoa uwe umejitoa muhanga.
Kwa yote hayo hapo juu, unafikiri hakuna mtu anayeweza kufanya vizuri zaidi?