Wapinzani Tanzania kumzodoa Raila ni kupoteza Dira na Mwelekeo

Wapinzani Tanzania kumzodoa Raila ni kupoteza Dira na Mwelekeo

Strong actions ni pamoja na Maandamano bwashee

Ndio unaona Mchungaji wa Iringa yuko Kenya kujifunza!

Ninakazia:

"Strong actions ni pamoja na maandamano kama mnufaika na katiba iliyopo anajivuta vuta kutupa anachotaka yeye na kwa wakati wake."
 
Ukizungumzia wapinzani unawazungumzia hawa walio nyuma ya keyboard huku JF?

Basi kama ni hivyo naona unakosea, mimi nadhani wapinzani ni viongozi wao wa vyama vya siasa, ambao wao sijui wanasemaje..

Mkuu miye ninawazungumzia wote kokote waliko, waliopo wenye kudhania Odinga ni mpuuzi, mkabila, kachoka, zee la hovyo, mwenye kutaka vurugu nk Kwa sababu zao zisizokuwa na mashiko.

Humo wano chawa, wafuasi, mashabiki, wanachama, viongozi nk.

Tusidanganyane, Kwa Odinga Kuna shule ya yaliyotushinda sisi.

Tulihitaji Odinga mmoja tu kuwa na katiba mpya miaka kama 30 iliyopita.

Leo tuko hapa tunachezeshwa ngoma ya maridhiano yaliyo siri.

(Sera za chama zinakuwa je siri --- JKN).

Kwa hakika Raila Amolo Odinga ni Jembe Ulaya la wakati wetu.
 
Ukivuliwa nguo chutama.🤣
nimetereza=nimeteleza.

Hakuna nguo yakuvua hapo. Unahangaika na kiswahili ukiwa kanda ipi mjomba?

Kiswahili kina baadhi ya maneno ambapo yote "l" na "r" yanakubalika.

Mojawapo ni "Tereza" na "Teleza."

Mengine ni kama kama "logwa" na "rogwa." Yako mengi ndugu nguchiro.

Kujiridhisha zaidi tembelea BAKITA Kijitonyama, au pia TATAKI iliyokuwa TUKI, UDSM Kwa msaada zaidi.

Habari ndiyo hiyo.
 
Utingo na kiingereza wapi na wapi ndugu?
Utingo wa kisasa....hata wewe na kusoma kwako bado ni utingo wa mwajiri wako. usingekuwa utingo kama ungekuwa unafanya kazi zako binafsi au umeajiri watu
 
Utingo wa kisasa....hata wewe na kusoma kwako bado ni utingo wa mwajiri wako. usingekuwa utingo kama ungekuwa unafanya kazi zako binafsi au umeajiri watu

Kwa mujibu wa kamusi ya TUKI utingo ni mmoja tu. Huyo hupatikana kwenye basi la abiria au Lori la mizigo na kazi yake imeelezwa waziwazi.

Wacha kuchanganya maneno bila rejea za kamusi rasmi, kama hili zezeta lenye Magonjwa Mtambuka.
 
Back
Top Bottom