Mimi ni wa Kanda ya Ziwa, na siamini katika Ukabila wala Ukanda.
Siamini kuwa SGR kwenda Mwanza badala ya Kigoma kuna manufaa kwa watoto wangu na wajukuu wangu.
Naamini katika haki.
Naamini katika Demokrasia.
Naamini katika usawa.
Ninaamini kuwa Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja.
Ndiyo sababu naamini kuwa SGR kwenda Kigoma kusafirisha mizigo ya Kongo, DRC, kuna tija zaidi kwa kizazi changu kuliko kwenda Kanda ya Ziwa kwa lengo la kubeba mizigo ya Rwanda na Uganda ambayo baadaye inaelekea huko huko DRC kuchochea machafuko