Wapinzani wa Nje: Acheni Tabia Mbaya ya Kuingilia Mambo ya Ndani ya Tanzania

Wakati sisi tunaingilia mambo ya nchi zingine ulikua bado kiunoni kwa baba yako!

Jielimishe hapa,


USHAURI WA ASKOFU KWA RAIS SAMIA JUU YA WANAHARAKATI WATOKAO NCHI ZA NJE!

Tarehe 19 Mei 2025 ni siku iliyokuwa imebana sana kwangu. Sikuweza kufanikiwa kufuatilia hotuba yeyote iliyotolewa na Mheshimiwa Rais Samia Saluhu Hassan. Hata hivyo, usiku niliona habari picha kadhaa zikiwa na maneno ambayo yanaelezwa kuwa yalitolewa na Rais Samia.

Katika habari picha mojawapo, Rais alinukuliwa akisema: "Tusitoe nafasi kwa wanaharakati wa nje kuingilia masuala ya Tanzania"! Kama kauli hiyo ni ya Rais Samia Saluhu Hassan, nchi yetu itakuwa imefikia hatua mbaya sana kwani hata Rais amejua kuwa tumefikia mahali ambapo tunahitaji watu au wanaharakati wa nje kutetea wananchi wa Tanzania.

Huko nyuma kuanzia mwaka 1961 hadi 1990, wanaharakati, wanasiasa na viongozi kutoka Tanganyika na baadaye Tanzania ndio ambao walikuwa wakiingilia masuala ya nchi jirani au nchi za nje. Wanaharakati, wanasiasa, watetezi na viongozi hao waliokuwa wakiingilia mambo ya nchi nyingine waliongozwa na Rais Julius Nyerere mwenyewe.

Wakati Rais wa Malawi, Dkt. Hastings Kamuzu Banda anatesa na hata kuua watu wake, nchi ya Tanzania sio tu kuwa iliingilia masuala ya nchi ya Malawi, bali pia iliwapa hifadhi watu na wakimbizi kutoka Malawi akiwemo mwandishi nguli aliyekuwa akiandikia gazeti la Daily News.

Wakati Idi Amini Dada alipoipindua serikali ya Uganda na kumuondosha madarakani Rais Milton Obote, Rais Nyerere aliingilia masuala ya Uganda, akaenda mbali zaidi akawa hifadhi Milton Obote, Yoweri Kaguta Museveni, nk.

Wakati Afrika Kusini ilipokuwa chini ya mfumo wa utawala wa ubaguzi wa rangi, Tanzania ya Rais Julius Nyerere iliingilia masuala ya Afrika Kusini kwa kuhamasisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya nchi hiyo ikatoa ardhi kwa wapiganaji wa Afrika Kusini.

Nchi nyingine ambazo ziliingiliwa wanasiasa, wanaharakati na wapiganaji wa Tanganyika na baadaye Tanzania ni pamoja na Rhodesia (sasa Zimbabwe), Msumbiji, Angola, Namibia, Algeria, nk.

Lakini pia hakuna asiyejua ya kuwa wakati wa utawala wa Mobutu Seseko wa Zaire (sasa DR Congo), Tanzania iliingilia masuala ya Zaire kwa kuwahifadhi Desire Kabila (Baba Ntwale) na mwanaye hadi wakafanikisha kumuondoa madarakani Rais Mobutu. Mifano haiishi kwani sio watu wengi wanajua kuwa wanajeshi wetu walikwenda katika Visiwa vya Commoro. Lakini kama walikwenda kutembea au walikwenda kula pikiniki, ajuaye ni Rais Kikwete na Jenerali wake Davis Mwamunyange.

Kama asilimia kubwa ya Watanzania wanajua ya kuwa upinzani unanyanyaswa nchini huku viongozi wao kama Ali Kibao wameuawa na wengine kama Soka, Kipanya, Chaula, Mlay, Mbise na Mdude wametekwa na hawajulikani waliko, hautarajiwi kuwa wanaharakati wa nchi za jirani wasijue kuwa kuna ufinyaji wa haki za msingi nchi ikiwemo haki ya kuishi.

Lissu alipigwa risasi 16 mchana kweupe akiwa katika majengo ya serikali yanayolindwa pia na serikali lakini hadi sasa hakuna mtu ye yote aliyekamatwa na wala hakuna uchunguzi wo wote uliofanywa hadi sasa. Lissu amekamatwa na kupewa makosa mazito kabisa duniani ya uhaini ambayo hatima yake ni kunyongwa hadi kufa. Katika mazingira kama hayo, haitarajii ya kuwa wanaharakati kutoka nje za nje watakaa kimya wasiingilie mambo ya Tanzania. Kama Tanzania ilitia sahihi mikataba ya kimataifa juu ya haki za binadamu, ni lazima itaingiliwa na wanaharakati kutoka nchi za nje.

Kama wao Rais Samia, CCM pamoja na serikali yake wanataka Tanzania isiingiliwe na watu au wanaharakati kutoka nchi za nje, basi wafanye mambo mawili. Mosi, waandike katiba mpya au wabadili katiba iliyopo ili wanyofoe kifungu kile kinacholinda haki za binadamu. Pili, wafanye haraka sana juhudi kuiondosha Tanzania katika mikataba yote ya kimataifa. Baada ya kufanya hivyo, waiondoe Tanzania kutoka katika Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Afrika Mashariki, COMESA, SADC, nk.

Wakimaliza kufanya yote hayo, ndipo Tanzania ivunje uhusiano wa Kibalozi katika nchi zote duniani na iwaite Mabalozi wake wote walioko katika nchi hizo, mwisho iwafukuze Mabalozi wote wa nchi za kigeni walioko Tanzania. Hapo ndipo itoe kauli ya kutokuingiliwa na wanasiasa na wanaharakati kutoka nchi za nje kwani sasa Tanzania itakuwa tayari ni Kisiwa cha Mbudya!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam, 20 Mei 2025; saa 3:45 asubuhi.
 
kwa akili zako mm na wewe na lipumbavu? Unaujuaje ushoga wa mtu kama nawe siyo shoga?

Yupo mahakamani anapambana na sheria za kipumbavu.

Kama kweli unaamini alishitakiwa kwa haki UNAWEWESEKA NN na mitusi hapa.
Wewe kula RUSHWA UVIMBIWE VIZUR KICHWA MAJI
Unajuaje ushoga wa mtu kama nawe siyo shoga . Una kichwa kikubwa akili ndogo. Ati nawe ni mpiga mbinja wa ccm?
 
Hahaha Tanzania mnajisifu kuwa nyie ni viongozi wa HARAKATI za ukombozi barani Afrika sasa tatizo liko wapi kwa wanao taka kuikomboa Tanganyika?

Au nyie mlifanya tofauti na wao?
 
Unajuaje ushoga wa mtu kama nawe siyoshoga . Una kichwa kikubwa akili ndogo. Ati nawe ni mpiga mbinja wa ccm?
ACHA APATE ADABU UNADHANI SERIKALI HII NI KAMATI KUU YA CHADEMA KWAMBA KILA MBWA ANAWEZA ROPOKA USENGE MPUMBAVU WEWE! UTASHUGHULIKIWA UTAKAVYOKUJA..
 

Wewe hujui siasa. Kwataarifa Tanzania tunaingilia sana siasa za wenzetu pia. Hukumbuki, JPM kwenda kumpigia kampeni Ondinga. Hatujawahi kuona Wakenya wakihutubia mikutano ya Kampeni Tanzania. Kulipotokea vurugu 2007, si ni JK ndiye alikuwa wa kwanza kwenda kujifanya Msuruhishi? Hata Samia slikwenda kufanya usuruhidhi Kenya kwenye uchaguxi uliopita. What are you talking about?

Ukienda huko RSA, Namibia na Zimbabwe, CCM huwa wanahudhuria mikutano ya kampeni kwenye hizo nchi in the Name of "The Sisters parties".
 
Bila ya Wanaharakati wa nje Samia labda saa hizi angekuwa mfanyakazi wa ndani huko Oman, Okello Mganda ndio Ali spark mapinduzi matukufu ya visiwani Zanzibar
View attachment 3339735

No. Samia ni Mwarabu. Ndiyo daraja lililopoteza. Mjomba wake ni Waziri huko Oman.

Ila cha kujiuliza zaidi ya Mme na hawa watoto tulioanza kuwadikia baada ya Magufuli kufa, kuna mtu yeuote anayewafahamu ndugu wa Maza? Inawezekana ndugu eote wakawa wako huko kwao Oman....Just thinking aloud.
 
Utakuwa mtoto wa 2000, TANZANIA imeingilia sana siasa za mataifa ya njr na ndio maana ni nchi yenye mchango mkubwa sana kwa mataifa jirani kukombolewa , unapo kuwa chawa pia uwe unajisomea somea
 
Chawa wa mama , majeshi ya JWTZ yalienda kufanya nini DRC?
 
Nasi tuwaache waisraeli na wapalestina na mambo yao, na ulaya njaa na maradhi yetu vinawahusu nini?
 
Nimeishia hapo " Tanzania ni taifa lenye utulivu na amani" Kuna neno limenitoka kinywani nikiliandika hapa nitapigwa ban bure.

Yaani vijana wanatekwa na kuuawawa na hakuna chochote kinachofanyika si mahakama, bunge Wala serikali kuchukua hatia alafu unathubutu kutamka hayo maneno hapo juu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…