Wapinzani wakivurugana wanafukuzana, CCM wakivurugana wanapatana na kuombana msamaha. Hii imekaaje?

WAPINZANI KAMA CHADEMA KILIVYOJAA WAHUNI NA MATAPELI KAMA MBOWE UNATEGEMEA WASAMEHEANE HAO? YAANI HAKUNAUPINZANI HAPO KUNAWAFANYA BIASHARA NA WAHUNI TU
Well, hebu fafanua in fact uhuni wa CDM na utapel wa Mbowe!! Inaonekana unaijua CDM vzr sana mkuu. Hebu tiririka huo uhuni na utapel wao tafadhali!!
 
Ukweli ni kwamba hata CCM wanafukuzana mfano Sophia Simba. Kuombana msamaha na kusameheana ni kwa sababu CCM kuna keki ya taifa inayoliwa ambayo ni vigumu kuiacha. Kama si hiyo keki akina January Makamba, Nape, mzee Makamba, mzee Kinana, Ngeleja na wengine wasingepiga magoti na kusamehewa. KEKI TAMU.
Na hili ndio jibu..... Hta mtu akikosa ubunge atapoozwa na ubalozi so jazba inashuka anasamehe. Bila maslahi hakuna mtu mzalendo kwa CCM
 
WAPINZANI KAMA CHADEMA KILIVYOJAA WAHUNI NA MATAPELI KAMA MBOWE UNATEGEMEA WASAMEHEANE HAO? YAANI HAKUNAUPINZANI HAPO KUNAWAFANYA BIASHARA NA WAHUNI TU
Umetumia herufi kubwa kwa haraka utadhani unakimbizwa.
AKILI ndogo ndizo zinakufanya ujibu ukakasi!!
 
Wapinzani hawana hela za kuwahonga wapinzani wenzao kama ccm wanavohongana vyeo na fedha pia hawana dola ya kuwaua wapinzani wao kama ccm wafanyavyo kwa wale wenye misimamo isio yumbishwa !
 
Na hili ndio jibu..... Hta mtu akikosa ubunge atapoozwa na ubalozi so jazba inashuka anasamehe. Bila maslahi hakuna mtu mzalendo kwa CCM
Kwa mantiki hiyo tutarajie kufukuzana na kuvurugana kwa upande wa wapinzani mpaka watakapo pata dola ndio wataanza kuomba radhi wakiadhibiwa!?
 
Ninachojiuliza zaidi ni kwamba je wapinzani wako tayari Kutoa msamaha wa dhati ikiwa wataombwa msamaha!? Mf. Watu kama Dr Slaa akiwaomba msamaha chadema na kuomba kurejea chamani atasamehewa na kupokelewa?
Lakini pia mf ndugu zito kabwe aombe kurudi chadema, je ataweza kusamehewa na kuaminiwa na chama kama ilivyokua kwanza!?
 
Wanabodi naomba mnisaidie kuelewa shida iko wapi, maana tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini, tumeshuhudia vyama tofautitofauti vya upinzani vikiibuka na kujipatia wafuasi wengi na hivyo na hivyo kuwa tishio kwa chama tawala.

Kwa kumbukumbu zangu ni kwamba ilianza nccr mageuzi ilipata umaarufu mkubwa sana siku za mrema na kutoa ushindani mkali sana kwa ccm hasa kwenye uchaguzi wa 1995.

Baada ya hapo ulizuka mgogoro mkubwa sana ndani ya chama hicho ambapo viongozi wakuu waliishia kuvurugana na kufukuzana na kukiumiza sana chama na kukiondoa kwenye ramani ya siasa za ushindani.

Ndipo ikafuata zamu ya cuf chini ya prof Lipumba na Maalim Seif, kama ilivyokua kwa nccr ingawa kwa huku bara cuf haikufikia ile nguvu ya nccr ya Mrema lakini taratibu ilianza mizozo ya ndani ambayo nayo haikuiacha CUF salama.

Kilele cha CUF kuvurugana tulikishuhudia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambapo mambo yaliyotokea yameifanya cuf isiaminike tena. Maana viongozi wakuu walivurugana na kufukuzana.

Kwa upande wa chadema ingawa walikuwa na nguvu za waziwazi tangia 2010, lakini pia wao hawakuwa na kinga dhidi ya hii changamoto ya kuvurugana maana tulishuhudia baada ya kumpokea lowasa chamani katibu mkuu alisusa na baada ya hapo tumeshuhudia matukio mengi ya fukuzafukuza ndani ya chama.

Ila kinachonishangaza ni kwamba ccm ina wanachama wengi sana, na mara kadhaa wamekua wakitifautiana kauli na mitazamo hata hivyo wao huitana kuombana msamaha na makaripio na maisha kuendelea.

Ni kwa nini wapinzani ni ngumu kumaliza tofauti zao kwa kusameheana na kuruhusu maisha yaendelee!?
Acha kudanganya, Membe mbona alifukuzwa CCM. Au ulikuwa hujazaliwa? Membe alitimkia Wazarendo
 
Kwa mantiki hiyo tutarajie kufukuzana na kuvurugana kwa upande wa wapinzani mpaka watakapo pata dola ndio wataanza kuomba radhi wakiadhibiwa!?
Wapinzani hawafukuzani bali migogoro huwa mingi kma fursa ni chache na hta CCM leo hii wakitoka madarakani expect wengi watahama maana hakutakua na vyeo vya hisani vya kufutana machozi.
 
Ninachojiuliza zaidi ni kwamba je wapinzani wako tayari Kutoa msamaha wa dhati ikiwa wataombwa msamaha!? Mf. Watu kama Dr Slaa akiwaomba msamaha chadema na kuomba kurejea chamani atasamehewa na kupokelewa?
Lakini pia mf ndugu zito kabwe aombe kurudi chadema, je ataweza kusamehewa na kuaminiwa na chama kama ilivyokua kwanza!?
Yes mbona Kafulila alirudi akasamehewa, Mkosamali amerudi kasamehewa, so haitokua mara ya kwanza msaliti kusamehewa.
 
Kwa hiyo siasa tanzania haziongozwi na dhamiri Safi bali zinaongozwa na njaa!?
 
Yes mbona Kafulila alirudi akasamehewa, Mkosamali amerudi kasamehewa, so haitokua mara ya kwanza msaliti kusamehewa.
Nakusudia wanapenda ccm hao uliowataja walihama lakini ilikuwa ndani ya upinzani maana ukijaribu kushauri dr Slaa arudi wadau wanafura sana!!
 
Chadema ni chama halisia.hawana madaraka,hawana hela lakini chama kinazidi kusonga Mbele.
clap.gif
 
Ninachojiuliza zaidi ni kwamba je wapinzani wako tayari Kutoa msamaha wa dhati ikiwa wataombwa msamaha!? Mf. Watu kama Dr Slaa akiwaomba msamaha chadema na kuomba kurejea chamani atasamehewa na kupokelewa?
Lakini pia mf ndugu zito kabwe aombe kurudi chadema, je ataweza kusamehewa na kuaminiwa na chama kama ilivyokua kwanza!?
Dr. Slaa hajafukuzwa CHADEMA bali alijitoa baada ya kutofautiana na wenzake. Kimantiki kwa vile suala walilotofautiana limeisha akitaka anarudi. Kuhusu Zitto mwenyekiti Mbowe ameshawahi kusema kuhusu kundi la covid 19 kuwa wakiomba radhi watasamehewa. Kwa hiyo yeye anaweza kusamehewa kama Sophia Simba alivyosamehewa.
 
Kwa Ndugai na ccm nilikuwa nangoja muda tu ili afanye alichokifanya leo ila wangekuwa wapinzani hapa Ndugai angekuwa tayari keshaitwa na kuambiwa ajieleze kwa nini asifukuzwe uanachama tena mbele ya media.
 
Wanabodi naomba mnisaidie kuelewa shida iko wapi, maana tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini, tumeshuhudia vyama tofautitofauti vya upinzani vikiibuka na kujipatia wafuasi wengi na hivyo na hivyo kuwa tishio kwa chama tawala.

Kwa kumbukumbu zangu ni kwamba ilianza nccr mageuzi ilipata umaarufu mkubwa sana siku za mrema na kutoa ushindani mkali sana kwa ccm hasa kwenye uchaguzi wa 1995.

Baada ya hapo ulizuka mgogoro mkubwa sana ndani ya chama hicho ambapo viongozi wakuu waliishia kuvurugana na kufukuzana na kukiumiza sana chama na kukiondoa kwenye ramani ya siasa za ushindani.

Ndipo ikafuata zamu ya cuf chini ya prof Lipumba na Maalim Seif, kama ilivyokua kwa nccr ingawa kwa huku bara cuf haikufikia ile nguvu ya nccr ya Mrema lakini taratibu ilianza mizozo ya ndani ambayo nayo haikuiacha CUF salama.

Kilele cha CUF kuvurugana tulikishuhudia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambapo mambo yaliyotokea yameifanya cuf isiaminike tena. Maana viongozi wakuu walivurugana na kufukuzana.

Kwa upande wa chadema ingawa walikuwa na nguvu za waziwazi tangia 2010, lakini pia wao hawakuwa na kinga dhidi ya hii changamoto ya kuvurugana maana tulishuhudia baada ya kumpokea lowasa chamani katibu mkuu alisusa na baada ya hapo tumeshuhudia matukio mengi ya fukuzafukuza ndani ya chama.

Ila kinachonishangaza ni kwamba ccm ina wanachama wengi sana, na mara kadhaa wamekua wakitifautiana kauli na mitazamo hata hivyo wao huitana kuombana msamaha na makaripio na maisha kuendelea.

Ni kwa nini wapinzani ni ngumu kumaliza tofauti zao kwa kusameheana na kuruhusu maisha yaendelee!?
Membe alifukuzwa au? Sophia Simba alifukuzwa au? Hivi waliombana msamaha yakaishia pale pale?
 
Dr. Slaa hajafukuzwa CHADEMA bali alijitoa baada ya kutofautiana na wenzake. Kimantiki kwa vile suala walilotofautiana limeisha akitaka anarudi. Kuhusu Zitto mwenyekiti Mbowe ameshawahi kusema kuhusu kundi la covid 19 kuwa wakiomba radhi watasamehewa. Kwa hiyo yeye anaweza kusamehewa kama Sophia Simba alivyosamehewa.
Inavyoonekana ni kwamba ndani ya upinzani kuna figisu nyingi sana kama ilivyo tu ndani ya ccm isipokuwa tofauti yao ni kiwango cha kuvumiliana. Inaoneokana huku upinzani uvumilivu unasomeka zero tolerance.
 
kwa sababu kuna wanafiki nawakweli hivyo sirahisi wakakaa pamoja,naukiona watu wanagombana kwa hoja kisha wanasema tumeyamaliza ujue mipango yao nimimoja wanachopishana ninjia tu! Utajuaje ? Angalia kati yawana ccm katafute kauli zake za kipindi cha maraisi kikwete,magufuli na sasa samia,hakuna mwenye kauli moja sasa watu kama hawa kwanini washindwe kumaliza tofauti zao?
Na ndivyo inavyotakiwa,huwezi kuwa na chama kila mtu kambale 😁😁
 
Back
Top Bottom