Wapinzani wakivurugana wanafukuzana, CCM wakivurugana wanapatana na kuombana msamaha. Hii imekaaje?

Inavyoonekana ni kwamba ndani ya upinzani kuna figisu nyingi sana kama ilivyo tu ndani ya ccm isipokuwa tofauti yao ni kiwango cha kuvumiliana. Inaoneokana huku upinzani uvumilivu unasomeka zero tolerance.
Pia kwa ccm unaweza kuahidi anaeleta chokochoko cheo aka mute.

Mwendazake zake alikuwa anawaambia wasihuzunike kuteua wapinzani kwani nafasi ziko nyingi Sana kwa ajili yao.
 
Kwani walifanyaje mkuu mwisho wa siku si wamekipigia magoti chama!!
Maelezo yako uliyoandika kwenye thread yako yanakinzana na ulichonijibu. Ndiyo maana nikauliza kuhusu wanachama wawili tu kama mfano kuthibitisha kwamba hata huko CCM fukuza fukuza ipo ilikuwepo na huwenda itakuwepo zaidi kwani hata yenyewe inaongozwa na watu

Unapoanzisha thread unapaswa kuwa na uthibitisho au ushahidi wa kutosha wa kutetea hoja yako pasi na shaka vinginevyo unachokuwa unaandika kitakuwa "mahaba Niue" kwa chama chako
 
Walio mshauri Mh Ndugai aombe msamaha bila kukiri kosa wasiishie hapo. Wamshauri ajiuzulu. Kitendo alichokifanya leo kimeshusha hadhi ya Bunge na Taasisisi ya Urais. Mataifa yatatushangaa kwamba hii ndio aina ya msamaha inayo mhusu Mh Rais na Amiri Jeshi Mkuu.
 
kinachonishangaza ni kwamba ccm ina wanachama wengi sana, na mara kadhaa wamekua wakitifautiana kauli na mitazamo hata hivyo wao huitana kuombana msamaha na makaripio na maisha kuendelea.
Ila kumbuka hawaachiani Maji mezani..."wamesameheana" publicly lakini sirini mambo si mambo!!
 
Vyama vya upinzani ni saccos za watu ndio maana wenyeviti ni walewale tu, ukitishia uenyekiti wa mmiliki wa chama ujiandae kufukuzwa ukikomaa sana maisha yako yaweza kukatizwa,bora ya CCM aisee
 

Wakiomba msamaha wa kweli wanasamehewa mchana kweupe. Ila sio rahisi waombe msamaha kwani huko upinzani hawana vyeo na ulaji wa kuwapa.
 
Labda wewe ndio hukuelewa hoja yangu, hoja yangu ni kwamba upinzani hakuna kuvumiliana hivyo makosa mengi sana hata ya kawaida huwa adhabu yake inakuwa kufukuzwa uanachama.
Mf suala lililopelekea kina silinde kufukuzwa uanachama lilikua suala la kipuuzi sana sidhani kama lile kosa wangelifanya walivyofanya chadema!!
 
CCM inawatisha wanachama.wake kwamba endapo wakikijeruhi chama basi dola Inawapa kichapo..

Kitendo cha Mkuu wa Muhimili ati kupiga goto kwa chozi ni aibu kubwa sana kwa Taifa.

Yaani naona afadhali ya Nape kuliko huyu mwamba..laah
 
Hiyo inaoonesha kukomaa kisiasa kwa CCM na wanaCCM.
 
Afu vyombo vya dola chini ya serikali yao ya CCM hutumika katika kutishana na hivyo kuwekana sawa na kujifanya wanaombana misamaha na hatimaye kusameheana.
Hawana lolote hao- wahuni tu.
 
Wanabodi tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini, tumeshuhudia ccm ina wanachama wengi sana, na mara kadhaa wamekua wakitifautiana kauli na mitazamo hata hivyo wao huitana kuombana msamaha na makaripio na maisha kuendelea.
p
 
Hata huyo Dr Slaa aliponyimwa nafasi ya kugombea uraisi kwa tiketi ya Chadema aliondoka.
Tuseme hata Dr Slaa hakuwa na subira bali alifuata kugombea uraisi.Na hiyo ingekuwa mara pili.
Ni Dr Slaa huyo huyo alitokea CCM baada ya kuondolewa jina lake kugombea ubunge.
Tofautisha Hussain Bashe alivyoondolewa jina lake tena akiwa kada maarufu lakini alibaki CCM.
Tuseme tu vyama vya upinzani kuna waliokuwa wapo humo as long watakuwa na madaraka au watagombea nafasi za juu.
Lakini wapinzani wanavurugwa na ukata ni rahisi kukisaliti chama,ongezea na mapandikizi.
 
Ila kumbuka hawaachiani Maji mezani..."wamesameheana" publicly lakini sirini mambo si mambo!!
Hilo la kutoachiana maji ni hulka ya mapambano kwani unadhani kule upinzani ndio wote huaminiana? Nani aliwahi kuwaza kwamba Halima mdee atakuja saliti chama? Lakini una uhakika gani na huyo aliye karibu nawe kwamba sio mamluki!?
 
WAPINZANI KAMA CHADEMA KILIVYOJAA WAHUNI NA MATAPELI KAMA MBOWE UNATEGEMEA WASAMEHEANE HAO? YAANI HAKUNAUPINZANI HAPO KUNAWAFANYA BIASHARA NA WAHUNI TU
Acha kumshambulia mtu binafsi. Mbowe ni baba yako kabisa. Kumwambia Mbowe maneno kama hayo ni sawa na kumwambia mme wa mama yako.
 
WAPINZANI KAMA CHADEMA KILIVYOJAA WAHUNI NA MATAPELI KAMA MBOWE UNATEGEMEA WASAMEHEANE HAO? YAANI HAKUNAUPINZANI HAPO KUNAWAFANYA BIASHARA NA WAHUNI TU
Embu! bila shaka yeyote na ili watu wajiridhishe taja uhuni wa Mbowe kwa ushahidi halisi usio tia shaka ! Ili kuondoa uongo ulio tengenezwa dhiidi ya Mbowe.
 
ccm wengi hawana maisha nje ya siasa, period!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…