Wapinzani wamepoteza Mwelekeo? Hawana Sera?

Kipindi cha Mkapa sukari ilikua bei gani ukilinganisha na sasa?

Petrol ilikua bei gani?

Mchele na vifaa vya ujenzi?

Kwa Mkapa ulilipa tozo yoyote kwenye simu?

Vipi kuhusu tozo ya majengo kwenye umeme?

Hujaona mabadiliko yeyote mkuu?
Kipindi cha mkapa wewe ulikuwa na umri gani na sasa una umri gani. Kipindi cha mkapa kulikuwa na population kiasi gani na sasa hivi iko kiasi gani? Kila kitu kinabadilika baada ya muda flani. Maswali mengine mpaka unajiuliza kama muulizaji kafika hata darasa la tatu
 
Inasikitisha sana hatuwezi kuwapa nchi waganga njaa!
 
Labda tuwape Makonda au Sabaya ndipo Chadema itaaminika kwa wananchi.
Tatizo la CHADEMA ni kuwakumbatia wageni wa nje kuwafanyia Propaganda. Na tatizo linakiwa kubwa kwasababu "marafiki wao wa Demokrasia" au vyama inavyoshirikiana nao, kwa sasa, wanaelemea to the far right. Ni mabaguzi na hawana interest yeyote ile na Jamii ya Mtanzania zaidi ya kutaka Rasilimali za Nchi hii.

Unawezaje kushirikiana na Vyama vya mlengo wa Kulia, tena wanaoapa kuwa Mwafrika sio binadamu, na sio hivyo tu, bali kumuangamiza fursa ikitokea.

Unafikiri haya matusi na uhasama dhidi ya Mwafrika(Mtu mweusi) ili kuamsha hisia zake yanatoka wapi? (Hiyo ni blue print yao, ni psychological warfare na sasa wamo humu, wamejazana Jamiiforums wakijinasibu kama Waafrika au Watanzania weusi, na wengi wao ni wanaharakati wa CHADEMA, ni mamluki! Unamwamini Vipi CHADEMA kutatua matatizo ya Mwananchi?

Tukirudi kwa Makonda na Sabaya. Unataka kusema hawa sio Waaminifu? Unataka kusema Rais mwenye kila aina ya ripoti za kijasusi-hamjui Makonda au Sabaya?

Sasa labda awe mtu wa kukariri kariri tu bila ya kudadavua Uhasama na malengo ya kampeni hii, ndio atapevuka ataona kana kwamba Rais hajui kitu, na kitakacho fuata kitakuwa ni kumsengenya na kumdhihaki Rais, na yote hayo yanaweza kuleta taswira potofu na madhara mengine kwenye Usalama wa Taifa letu.


Ni nani ambaye unafikiri atakuwa nyuma ya Propaganda hizi?
 
Hivi CCM huwa hawana cha kuzungumza mbali na kuiongelea Chadema? Mara Chadema imekufa mara Chadema hawana sera lakini muda wote wanaiongelea Chadema
Ume hesabu nyuzi zenu za Makonda na CCM?

Hata hivyo, CHADEMA haina sera na Uongozi wake Umekufa
Hivi CCM huwa hawana cha kuzungumza mbali na kuiongelea Chadema?
Hata isipoongelewa au kuzungumziwa, CHADEMA ni puppets wa mabeberu.
 
hawana viongozi mahiri, wenye maono, dhamira na nia ya dhati ya kuwakomboa waTanzania πŸ’

kwa tamaa na uchu wa madaraka miongoni mwao, uhasama na uadui wa wazi kabisaaaa baina yao, ubinafsi na kutoaminia wao kwa wao, kumewafanya wawe dhaifu na kibogoyo zaidi πŸ’

mathalani,
wakizungumzia umoja,
waTz wanajiuliza wameshindwa kuungana wao kwa wao na kua upinzani moja wenye nguvu, then huo umoja gani wanazungumzi?

ooh waTanzania watuaminiπŸ’
Nani atawaamini wapinzani ambao hawaaminiani wao kwa wao?

Ooh tutarekebisha uchumi πŸ’
mtarekebishaje uchumi upi na hamuoneshi mipango mikakati mbadala na mmeng'ang'ana na masuala ya vyeo tu na nafasi za uongozi. Na hapo ndipo mnaweza kujieleza vizuri lakini sio kwenye uchumi. Mmestukiwa na wanainchi πŸ’

kwa ujumla upinzani umekosa uelekeo, umekosa dira, umekosa sera, umekosa mipango na mikakati ya kumvutia na kumshawishi mwanainchi walau awasikilize tu πŸ’

mbaya zaidi kuingia kwa vibaraka walotumwa na mabwenyenye wa ng'ambo wameudhoofisha na kuumega zaidi upinzani. Upinzani umekua na sura ya ukoloni mambo leo πŸ’

still we have time,
we can organize united, trusted, committed, focused and vibrant opposition hr in Tz, should we be real and true patriotics πŸ’
 
Ume hesabu nyuzi zenu za Makonda na CCM?

Hata hivyo, CHADEMA haina sera na Uongozi wake Umekufa

Hata isipoongelewa au kuzungumziwa, CHADEMA ni puppets wa mabeberu.
Sasa kwanini msikifutie usajiri. Bashite lazima asemwe ili vizazi vimjue rangi yake halisi,maana mzaha mzah Jiwe akawa Rais
 
Sasa kama upinzani umekosa yote hayo mbona kutwa mnapoteza muda kuwajadili badala ya kufanya yenu?
 
Sasa kama upinzani umekosa yote hayo mbona kutwa mnapoteza muda kuwajadili badala ya kufanya yenu?
kwasabb inahitajika kua na vibrant opposition na ni haki ya kikatiba kwa TanzaniaπŸ’

sio hii ya kudai uchaguzi huru wa kitaifa hali ya kua chaguzi kwenye vyama vya Upinzani ni figisu, kiza totoro ni hatari kwa afya na uhai wa wanachama πŸ’

wanadai Demokrasia na uhuru hali ya kua kwenye vyama vya ni udictator, ubabe na Mapinduzi kila uchwao πŸ’

wanadai haki, uwazi, uwajibikaji na usawa hali ya kua kwenye vyama vyao ni kichekesho 🀣

ni muhimu kuzingati hoja ya Upinzani dhaifu na kibogoyo πŸ’
 
Sajili chama tutakuunga mkono
 
Kama ni kweli basi wananchi hawawezi kuwachagua, sasa kwanini CCM wanaogopa tume huru ya uchaguzi ili hali Wananchi wana imani na nyie ambao mko na sera na muundo mzuri? Mlivyo waoga eti mmebadilisha jina tu wakati muundo bado ni ule ule. Kila mtu akielimika tu hata kidogo huwezi mwambia habari za CCM labda awe na maslahi binafsi. Kuna wale huwa wanasema bora CCM iendelee kutawala maana wapinzani wataleta vita πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Ukiangalia maisha yake hajui hata kuwa ile picha ya Yesu siyo halisi au kama kuna vita kati ya Ukraine na Urusi. Yaani kwa kifupi ni wale wasio na taarifa yoyote wala hajui umasikini wake umetokana na hiyo CCM.
 
Kwahiyo na wewe unaona maisha ni yale yale, hakuna mabadiliko?

Kwamba kipindi cha Mkapa na sasa ni sawa?
 
Sawa Maarifa kuna jambo lingineπŸ€”
 
Kwahiyo na wewe unaona maisha ni yale yale, hakuna mabadiliko?

Kwamba kipindi cha Mkapa na sasa ni sawa?
Hapana mkuu,na hakuna sehemu nimesema kuwa maisha ni yale yale,je unaweza kunionyesha wapi nimesema maisha ni yale yale?
 
Lema anadhani Makonda anakuja kumuondoa kwenye ushindi wa ubunge.
Anasahau yule siyo mgombea ubunge Arusha bali mtendaji wa serikali.
 
Kama unataka wawaze na kunena kama unavyowaza wewe umepotea. Jua kuwa wewe si mwenye definition ya kipi ni hoja na kipi sio. Unawachagulia cha kusema kama nani? Waache waendeshe mambo yao waonavyo inafaa. Wewe myuvisisiemu inakuuma nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…