Wapinzani wamepoteza Mwelekeo? Hawana Sera?

Wapinzani wamepoteza Mwelekeo? Hawana Sera?

Kipindi cha Kikwete walipinga sana suala la Ufisaidi. Hili walilisimamia kidete kwa kweli tunashukuru lilisikika maana ni kweli lilitamaraki.

Kipindi cha Magufuli chorus ilibadilika ikawa ni Makonda hivi Makonda vile. Wakalalamika tu Magufuli ni Dikteta n.k. Magufuli akafariki.

Wakajaribu kusikilizia upepo haukwenda sawa. Wakaja na suala la Katiba mpya. Likaenda enda wakaliacha. Hawajawa na consistency katika hili jambo la msingi sana. Wameiacha hoja hii ya msingi ya Katiba Mpya.

Sasa wanadakia na kusimamia kila tamko linalosemwa na wanasisiem. Na hasa hasa matamko ya Makonda. Inashangaza. Hawana tena data mbalimbali za msingi za kuelezea ufisadi ambao unafanyika. Hawana muda wa kuelezea madhambi mbalimbali na mapungufu wanayoyaona.

Watanzania wana maisha magumu hakuna wa kuwasemea. Kwa sasa kila mtu anaimba wimbo wake. Lema amekazana na kauli ya Makonda ndo imekuwa sera yake. Hana jipya.

Lini tutapata upinzani imara wa kweli? Mwacheni Zitto yeye anakula pension. Huyo msimguse yupo ICU. safari hii hana cha kukosoa.
Ccm Wana mwelekeo mzuri ndio maana tuna umeme wa kutosha
Tuna Dola za kutosha, deni la taifa tril 90 zinahimilika na kikokotoo Cha 30% kipoo sawa tu.

Kimsingi watz wote tupo happy na ccm
 
Wenyeviti wa upinzani wamechoka. Hawana mbinu wala sera yoyote mpya. Wengi wameongoza zaidi ya miaka 20. Wako hoi kifikra.
Huenda ulingo wote wa siasa umekwama,mkate mezani ndo jibu sahihi,hivi sasa Hali ya familia nyingi ni ya hovyo
 
CHADEMA sio chama cha kutiliwa maanani na Mtanzania yeyote yule.

Ukiwa una viongozi muda wote ule wao wapo kutukana tu, utasikia vipi au wapi Sera zao?

CHADEMA inahitaji Mwenyekiti, damu mpya mwenye uwezo wa kuongoza viongozi wenzake wawe focus na kutafuta masuluhisho ya makali yanayowapata Wananchi. Wanahitaji kuuza sera.

Mbali ya CHADEMA, vyama vingine vya Siasa vimekuwa kama wasindikizaji wa ngoma ya mdundiko tu.
Yaani upinzani apate soln ya mabalaa wanayopata wananchi?? Umeme tabu, maji hakuna, madawa hakuna, pesa ndio hizo ripoti ya CAG kila leo inaonyesha mabilioni yanaliwa na hakuna hatua zinazochukuliwa!! Watanzania ni wa kuachwa na kufa tu hadi kizazi kipya kitakacho kuja chenye kujitambua.
 
Back
Top Bottom