Wapinzani watakaoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa ni wasaliti wa watanzania

Wapinzani watakaoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa ni wasaliti wa watanzania

Chief Kabikula

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2019
Posts
7,567
Reaction score
9,037
Baada ya juzi kuandika uzi wenye kichwa cha habari hapo juu, naona Chadema kwa mara ya kwanza wamefanya uamuzi sahihi sana wa kutoshiriki kuhalalisha uchaguzi haramu uonekane halali, pongezi sana kwao sasa ni zamu ya vyama vingine kutoubaliki uchaguzi huu haramu, Zitto Kabwe na Act Wazalendo yake mpira uko mkononi mwako kututhibitishia watanzania kuwa wewe ni mtu wa kitengo mjasilia siasa kama ulivyotuhumiwa na Chadema wakati unafukuzwa au ni mpinzani wa kweli. Watanzania sio wajinga wanakuangalia tu waone nini utafanya, bora afanye Lipumba lakini sio wewe.
 
Kwanza hiyo ACT ndio mfu kabisa bora hata dovutwa
 
Tanzania kuna vyama vingi vya siasa

CUF na TLP wanashiriki

Wengine wameogopa kushindwa
Praise team wa kusifu na kuabudu mmevamia uzi kifupi Chadema haishiriki kuhalalisha uchaguzi haramu uonekane halali, mnaumia nini si mtapata ushindi zidi ya wenza CUF na TLP.
 
Ninyi madikteta wakubwa, mnalazimisha maamuzi yenu ya uoga yaigwe na vyama vingine utafikiri mnawagawia ruzuku!

Kila mtu apambane na hali yake
ACT Wazalendo wakijitoa si ndio mtapita bila kupingwa nchi mtakuwa mmeifikisha uchumi wa kati.
 
CHEKESHO !!!
SUSENI SIYE TWALA , yaani mnamalengo ya kujenga nyumba alafu mnakataa kujenga msingi !!!
Sasa mnaumia nini Chadema kujitoa kama mnakula. Haya kuleni na mapandikizi yenu ya kitengo mliyoyaweka upinzani.
 
Kwa Zito kususa sijui, labda kwa nguvu za maalim.
 
Huyo Zitto asibembelezwe kujitoa, akiona mchakato sio sawa anaweza kuamua atakacho aendelee kushiriki au ajitoe. Lakini watu wanaopigia kura upinzani wanajitambua hivyo hatuwezi kushiriki ushenzi wa aina yoyote.
 
Back
Top Bottom