Wapo wanaosema wanawake wakae nyumbani kutunza familia na wapo wanaosema mwanamke afanye kazi. Tuwekane sawa

Wapo wanaosema wanawake wakae nyumbani kutunza familia na wapo wanaosema mwanamke afanye kazi. Tuwekane sawa

Bolotoba

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2024
Posts
3,424
Reaction score
7,706
Sasa A. Proposers wanasema mwanamke afanye Kazi.

1. Na hoja yao ya msingi ni 50/50 kimajukumu.
2. Hoja ya nyongeza ni wanawake wafanye kazi ili kujikeep busy.

👉 kundi hili wanasema mwanamke anae kaa nyumbani ni rahisi kufanya ufuska lakini pia ni mzigo (wahenga wakisema an idle mind is the workshop of devil)
Wanajenga hoja nyingine je mwanaume akitangulia mbele za hali je? 🤔mke atawahandle watoto vipi kama hakuwa na kazi

👉Na je hawa wanawake wenye degrees na diploma walienda Chuo kwa minajiri gani?

B. Kundi hili ni opposers wao wanasema mwanamke hatakiwi kufanya zaidi ya kulea nyumbani na kufanya domestic activities

👉Kundi hili Wanajenga hoja kuwa mwanamke kufanya kazi ni kuingilia majukumu ya mwanaume
👉Kundi hili linaenda mbali zaidi na kusema kuwa mwanamke anapokuwa mbali na nyumbani Yani kazini anapata mwanya wa kucheat na wafanyakazi wenzie

Sasa wakuu tuwekane Sawa kuna mkanganyiko mchuano ni mkali maana wapi kuna unafuu wanawake wa nyumbani vs wanawake wa makazini?

Naunga mkono hoja (opposers).
 
Je, unaamini katika 400 wote walikuwa waajiriwa? Kumbuka kuna mke wa pastor kwenye list tunaamini huyu si muajiriwa. Naamini wapo wengine pia ktk list ambao ni mama wa nyumbani.

Unachotakiwa kujua ni kwamba unapoingia kwenye ndoa yeyote anaweza kucheat, awe mwanamke awe mwanaume., anaekaa home au anaefanya kazi. Uaminifu hauko promised wala guaranteed kwenye ndoa. Know this and know peace.

Kuna wamama wa nyumbani ukielezwa machafu yao hutaamini. Acha kila mtu afanye kinachompendeza.
 
Turudini kwenye asili ya uumbaji tangu awali. Ndipo tutapunguza kulialia ovyo. Hata nature ya miili yetu ME na KE jinsi tulivyoumbwa inatuhukumu.

50/50 na mambo ya usawa, ni mpango wa shetani tangu edeni huko kuharibu taasisi ya ndoa na amefanikiwa pakubwa sana. "Ukila hili tunda utakuwa sawa na Mungu" alisikika shetani akimshawishi eva habari za kuwa sawa na Mungu yaani atatoka 50/50 na Mungu😁😂 kama akila lile tunda. Ukitaka kuvuruga mengi we vuruga familia, matokeo yake utayaona kuanzia mtaa mpaka kitaifa.
 
Mimi namkataa mwanamke,

Na kazi zake zote,

Na mambo yake yote,

Najitoa kuwa wako, Ee pesa sabuni ya roho,

Nikutafute, nikutumie kwa uaminifu hata ninapokufa. AMEN.

Akae nyumbani au asikae, pingu za maisha na mwanamke ni mchezo hatarishi sana. Umeonywa.
 
Turudini kwenye asili ya uumbaji tangu awali. Ndipo tutapunguza kulialia ovyo. Hata nature ya miili yetu ME na KE jinsi tulivyoumbwa inatuhukumu.

50/50 na mambo ya usawa, ni mpango wa shetani tangu edeni huko kuharibu taasisi ya ndoa na amefanikiwa pakubwa sana. Ukitaka kuvuruga mengi we vuruga familia, matokeo yake utayaona kuanzia mtaa mpaka kitaifa.
Unaweza toa ushahidi logically kutetea hoja yako?
 
Ngoja nikupe siri Mimi na mke wangu mtarajiwa hatutafanya kazi baada ya ndoa tutakaa nyumbani tu pamoja na watoto wetu tutaajiri wafanya kazi sisi tutakuwa kama maboss tu, 😊
🤣🤲
 
Wao kazi ya kuzaa inawatosha mengine watuachie wanaume, Huwa umaarufu na pesa ni vitu hatari sana kwa wanawake wengi.
 
Wanaume waache konakona
Hupendi mtumishi kina dada jobless/watu wa biashara wapo wengi oa huko
Kila mtu achague kinachomfaa
 
Mtu asiye na uwezo wa kufanya kazi na Mtegemezi ni mzigo mkubwa sana katika familia - anazungumza Arkad katika kitabu cha The Richest man in Babylon

Kila mmoja anatakiwa kuwajibika katika Ndoa/familia ili kufikia uhuru wa kifedha kwa urahisi, Hata ikitokea mmoja akiondoka wengine wanaendelea kuwajibika bila kuyumba ...
 
Sasa mkuu wewe mwanamke unaweza kumwambia akaje na mboga, ahemee Mchele, Unga, sjui mafuta??
Mtu asiye na uwezo wa kufanya kazi na Mtegemezi ni mzigo mkubwa sana katika familia - anazungumza Arkad katika kitabu cha The Ricgest man in Babylon

Kila mmoja anatakiwa kuwajibika katika Ndoa/familia ili kufikia uhuru wa kifedha kwa urahisi, Hata ikitokea mmoja akiondoka wengine wanaendelea kuwajibika bila kuyumba ...
 
Sasa mkuu wewe mwanamke unaweza kumwambia akaje na mboga, ahemee Mchele, Unga, sjui mafuta??
Yaah sahihi mkuu, Kwamimi mwanamke ndio inatakiwa aende sokoni ...
Nitafute pesa ya familia nianze na kufikiria na kununua sukari, hiyo ni responsibility yake ....!!

Yako mazingira yatayonitaka mimi kununua hayo mazagazaga, ila haitakiwi wawe wananisubiria mimi ndiyo nirudi na vya kupika ....!!
 
Kwa hela yake??

Back
Top Bottom