Sasa A. Proposers wanasema mwanamke afanye Kazi.
1. Na hoja yao ya msingi ni 50/50 kimajukumu.
2. Hoja ya nyongeza ni wanawake wafanye kazi ili kujikeep busy.
👉 kundi hili wanasema mwanamke anae kaa nyumbani ni rahisi kufanya ufuska lakini pia ni mzigo (wahenga wakisema an idle mind is the workshop of devil)
Wanajenga hoja nyingine je mwanaume akitangulia mbele za hali je? 🤔mke atawahandle watoto vipi kama hakuwa na kazi
👉Na je hawa wanawake wenye degrees na diploma walienda Chuo kwa minajiri gani?
B. Kundi hili ni opposers wao wanasema mwanamke hatakiwi kufanya zaidi ya kulea nyumbani na kufanya domestic activities
👉Kundi hili Wanajenga hoja kuwa mwanamke kufanya kazi ni kuingilia majukumu ya mwanaume
👉Kundi hili linaenda mbali zaidi na kusema kuwa mwanamke anapokuwa mbali na nyumbani Yani kazini anapata mwanya wa kucheat na wafanyakazi wenzie
Sasa wakuu tuwekane Sawa kuna mkanganyiko mchuano ni mkali maana wapi kuna unafuu wanawake wa nyumbani vs wanawake wa makazini?
Naunga mkono hoja (opposers).